Na: Siwema Malibiche
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo (SUA) wamefanya matendo ya huruma kwa watu wenye uhitaji iliyohusisha walemavu, wajane na wazee
wasiojiweza wilayani Mvomero katika Kijiji cha Wami Sokoine.
Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti
wa Kamati ya Wanawake Chama cha Wafanyakazi RAAWU Tawi la SUA Bi Enessa Mlay amesema matendo hayo ya huruma ni matendo
yanatoa nafasi ya kuwasaidia watu wasiojiweza wenye uhitaji na kwamba yana
thamani kubwa kwa kusaidia na kuwafariji watu wasiojiweza.
Akizungumzia
mambo ambayo yamefanyika katika matendo hayo Bi Mlaya amesema wamepeleka nguo za aina zote zikiwemo
nguo za kike na za kiume pamoja na nguo za watoto, chumvi, sukari, unga, sabuni
na vitu vingine kutegemeana na jinsi wafanyakazi wa SUA wamejitokeza katika
kufanikisha matendo hayo
Amewataka Wanawake kuwa na uangalifu
mkubwa katika malezi ya watoto na wakisimamia mienendo sahihi katika elimu kwa
watoto kwani kupitia elimu itasaidia kuzalisha wataalam bobezi na weledi
watakaoisaidia Tanzania kupata maendeleo kupitia sekta mbalimbali iliwemo ya
kilimo.
Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii
wilayani Mvomero Bi. Pelice Lumambo amewashukuru wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA kwa kuwatembelea na kutoa chchote walichonacho kwa watu
wasiojiweza ndani ya Kijiji cha Wami Sokoine.
Naye Mkazi wa kitongoji wa Sokoine
Kanisani Pili Hassan ambae ni miongoni ya
mmoja waliofikiwa na matendo hayo ya huruma amewashukuru wale wote
waliojitoa kuwasaidia chochote walichojaaliwa na amewakaribisha wakati mwingine
kutosita kuwatembelea Kwani wanajiskia faraja kuona kuwa Kuna watu
wanawakumbuka na kuwajali.
Akizungumza katika tukio hilo Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Sokoine Kanisani Bw Omary Kapiato amewatoa hofu wale wote
wanaoishi katika mazingira magumu kuwa kuna watu wanawajali na kuthamini kama ambavyo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
SUA kimefanya kupitia wafanyakazi wake .
0 Comments