Wednesday, 11 October 2017

MKUTANO WA MENEJIMENTI YA CHUO NA MENEJIMENTI YA BENKI YA CRDBBenki ya CRDB imetangaza bidhaa yao mpya iitwayo “Salary Advance” kwa Watumishi wa umma ambapo ilifanya mkutano wake na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo siku ya Jumatatu tarehe 09/10/2017.
Mwenyekiti wa Mkutano huo Prof. Y.M. Ngaga, Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha ) alifungua mkutano huo kwa kumtambulisha Kiongozi wa msafara wa Menejimenti ya Benki  Bi. Grace Maseki, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la SUA ambaye aliongozana na Viongozi mbalimbali kutoka Makao makuu ya Benki ya CRDB.

Bidhaa hiyo ya “Salary Advance” inatolewa kwa wafanyakazi wa serikali ambao mishahara yao inapitishiwa katika akaunti za benki ya CRDB ambapo riba ya mkopo huu ni asilimia 5 tu ya mkopo unaokopwa na riba hiyo inakatwa kabla ya mkopo kutolewa hivyo mshahara unapotoka kiasi unachokatwa ni kiwango cha mkopo tu uliokopa.

Imeelezwa na maafisa hao kutoka CRDB kuwa,  vigezo vya kumfanya mtumishi huyo wa serikali kupata mkopo huo ni kwa mfanyakazi ambaye mshahara wake unapitia benki ya CRDB ili utakapokopa iwe rahisi kurejesha deni wakati mshahara unapoingia, uwe umejiunga na huduma ya “CRDB Simbanking” ambayo ndio njia rahisi ya kuupata mkopo wako na kuweza kulipa deni la mkopo wako.