Na Nicolaus Roman
Imeelezwa kuwa usomaji ni kitu muhimu katika maisha ya kila siku kwa Binadamu hasa
anaposoma kitu chochote chenye faida kwake na kwa jamii jambo linaloweza kuleta maen
deleo kwa Taifa.
![]() |
PICHA KUTOKA MTANDAONI |
Hayo yameelezwa na Bi. Editha Njau Msimamizi wa Kitengo cha Huduma ya Marejeleo
na Taarifa kwa Jamii katika Maktaba ya Taifa ya Kilimo iliyopo ndani ya Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA) wakati akizungumza na SUA Radio kwenye kipindi cha Kapu
la Leo.
Amesema taarifa sahihi hupatikana kwa kusoma na kupitia machapisho mbalimbali
ambayo yameandaliwa kwa usahihi hasa na wataalamu yenye lengo la kuelisha kitu
chochote kile ambacho mtu anatarajia kupata matokeo chanya.
Bi. Editha amesema Maktaba ya Taifa ya Kilimo SUA ipo kwa ajili ya kumsaidia
mwananchi kufahamu mambo mbalimbali yatakayo mletea faida hususani katika kilimo,
uvuvi, usindikaji, biashara na ufugaji na lengo la machapisho hayo ni kuhakikisha mtanza
nia anapata taarifa sahihi na kuweza kuzalisha kwa tija.
“Ukiwa unasoma machapisho mbalimbali mara kwa mara utakuwa mbunifu katika eneo
lako ulilopo kwa sababu kumbuka yale machapisho yameandikwa na wataalamu baada tu
ya kufanya utafiti, hivyo wewe unapokuja kusoma unapata taarifa na maarifa”, amesema Editha Njau
Aidha amesema ni muhimu kwa vijana kuwa na tabia ya kujisomea kwa kuwa
wanaposoma wanaongeza maarifa pia uwezo wao katika kufikiri unakuwa mkubwa na
utawapelekea kuwa wabunifu.
Kwa upande wake Msaidizi katika Kitengo cha Marejeleo na Taarifa kwa Jamii Bw.
Ismail Chibunda ambaye ni Msimamizi amesisitiza watu wote kuanzia watoto hasa
wakazi wa Morogoro wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kujisomea kwa kuwa kwenye
kusoma ndio maarifa yalipo na Maktaba ya Taifa ya Kilimo iliyopo SUA ni kwa ajili ya
kila mtu si wanafunzi pekee.
0 Comments