Na: Tatyana Celestine
Mhe. William Kipchirchir Samoei Ruto leo Septemba 13, 2022 amekula kiapo kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Kenya kwenye uwanja wa Moi Kasarani katika sherehe iliyosimamiwa na Msajili wa Idara ya Mahakama Anne Amadi na kushuhudiwa na Jaji Mkuu Martha Koome .
“Mimi, William Samoei Ruto, kwa kutambua kikamilifu wito wa juu ninaochukua kama Rais wa Jamhuri ya Kenya, naapa kwamba nitakuwa mwaminifu wa kweli kwa Jamhuri ya Kenya, aliapa rais mpya William Ruto.
Martha Koome baadaye alimwalika Rais anayeoondoka madarakani Mhe.Uhuru Kenyatta, akiandamana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya Jenerali Robert Kibochi kumkabidhi zana za Mamlaka ambazo ni Katiba na Katiba.
Viongozi wa mataifa zaidi ya Ishirini akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wameshiriki katika sherehe hizo za uapishwa wa Rais wa Tano wa Kenya Mhe. William Ruto
KATIKA VIDEO
0 Comments