Na.Vedasto George/ Tatyana Celestine
Wazee
Mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuwapatia pensheni jamii kama ilivyo
kwa wazee wa Tanzania visiwani Zanzibar ili waweze kujikimu katika maitaji yao
muhimu ikiwemo malazi, afya na chakula pia kuwapatia wawakilishi wa wazee
kwenye vyombo vinavyotoa maamuzi hapa nchini.
Mgeni Rasmi ambaye ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Morogoro Dkt. Masumbuko Igembya akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Morogoro katika Maadhimisho ya siku ya Wazee duniani yaliyofanyika Wilayani Mvomero Morogoro jana. (Picha na Tatyana Celestine).
Akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Morogoro Samweli Mpeka amesema endapo serikali ya Tanzania itawapatia pensheni jamii itasaidia kuondokana na changamoto zinazo wakabili hususani za kimatibabu ambapo wawee wengi nchini ukosa matibabu yaliyo sahihi kutokana na kutokuwa na kipato.
“Wazee wanao nufaika na pensheni ni wale tu walio kwenya mfumo rasimi ambao ni sawa na asilimia 4 ya wazee wote asilimia 96 ya wazee wengine ambao wamelitumikia taifa la Tanzania na kuweza kulipatia mafanikio na maendeleo haya tuliyonayo sasa kupita sekta isiyo rasimi ya ajira binafsi ikiwemo kilimo,Uvuvi,Ufugaji na biashara hawapati pensheni ya haina yeyote”. Amesema Samweli Mpeka Mwenyekiti wa wazee mkoa wa Morogoro.
Nae mgeni aliyemuwakilisha Mganga Mkuu Mkoa wa Morogoro katika maadhimisho hayo Dkt. Masumbuko Igembya amesema katika Mkoa wa Morogoro kuna wazee zaidi ya 100,000 (laki moja) huku wazee zaidi ya 40,000 (elfu arobaini) tayari wamepatiwa vitambulisho kwa ajiri ya matibabu bure sawa na asilimia 31 pekee.
“Kupitia Maadhimisho haya naomba kutoa rai kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri zote Mkoa wa Morogoro kuendelea na zoezi la kuwapatia vitambulisho vya matibabu wazee hawa ivyo kila halmashauri iweze kujipanga kwa kununua vifaa vyote vinavyosaidia kuweza kutoa vitambulisho ivi ili kila mzee ndani ya mkoa wetu wa Morogoro aweze kupatiwa kitambulisho”. Amesema Dkt. Masumbuko
“Lakini katika Mkoa wetu wa Morogoro tumeendelea kuboresha Afya za wazee kwa kutenga madirisha ya matibabu ya wazee na kuweka matangazo ya mpishe mzee apate uduma kwanza naili tumeweza kulishuudia katika vituo vyetu vya kutolea uduma linatekelezwa kwa umakini mkubwa Kwa mwaka 2019 hadi mwaka 2020 jumla ya misamaha ya matibabu iliyotolewa kwa wazee kwa mkoa wa Morogoro ni zaiodi ya misamaha elfu 27”. Amesema Dkt. Masumbuko
Awali akizungumza katika Kipindi cha Mchakamchaka cha suafm Naibu Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia Prof. Fatihiya Massawe amesema kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine kimeona umuhimu wa siku ya wazee duniani kwa kuona mchango wao mkubwa katika ujenzi na maendeleo ya taifa hivyo kupitia ndaki hiyo wataendele kutoa elimu kwa wanajamii ili kujiandaa na maishaya uzeeni iwasaidie kukabiliana na changamoto wanazozipata wazee wa leo.
Vile vile ameongeza kuwa sua kwa kuungana na wadau wengine duniani imejitoa kushiriki katika kutoa taarifa stahiki kwa jamii hasa zinazohusu wazee na jamii kwa ujumla ili kuwajali,kuwathamini na kuwatunza wazee kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyojieleza.
Siku ya wazee uadhimishwa kila mwaka na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuelimisha na kujenga hamasa kwa jamii katika kuboresha upatikanaji wa huduma na haki za wazee ili kuwa enzi.
0 Comments