SUAMEDIA

Serikali imezitaka Taasisi za Elimu Juu kuzingatia vipaumbele vya kitaifa kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya, Kilimo, Mifugo pamoja na Utalii.

 

 Na Vedasto George

SUA

Serikali imezitaka Taasisi za Elimu Juu nchini kuakikisha zinaazisha programu za masomo ambazo zitaendana na vipaumbele vya  kitaifa ili kuweza kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya, Kilimo, Mifugo pamoja na Utalii. 


  Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  Prof. James Mdoe akizungumza na Wathibiti Ubora Vyuo Vikuu hawapo pichani

Kauli hiyo imetolewa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  Prof. James Mdoe mkoani Morogoro  wakati akifungua jukwaa la siku mbili la  wathibiti ubora vyuo Vikuu  nchini (TUQAF) .

Amesema uanzishwaji wa programu zinazoendana na vipaumbele vya taifa zitasaidia kuzalisha wataalamu watakaoweza kuendesha na kusimamia  miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ya Kilimo, Afya, Mafuta pamoja na Gesi.

Aidha Prof. Mdoe amesema  kuwepo kwa Idara ya Uthibiti Ubora katika vyuo vikuu nchini itasaidia  kuimalisha Sekta ya Elimu, Uchumi wa Taifa pamoja na maendeleo ya jamii.


 Wathibiti Ubora Vyuo Vikuu wakisikiliza mada mbalimbali

Akizungumzia dhamira ya kuwepo kwa jukwaa hilo  Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU  Prf. Dominic Kiampa amesema  kukutana kwa wathibiti ubora wa vyuo vikuu kwa siku  mbili ni kujadili  na kutathimini miongozo mbalimbali iliyotolewa na  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na kuakikisha miongozo hiyo inatekelezwa ipaswavyo.

Kwaupande wake Makamu Mwenyekiti  wa jukwaa la  wathibiti ubora Vyuo Vikuu  Tanzania  (TUQAF) Kutoka Chuo Kikuu cha  taifa cha Zanzibar IDDI ALI amesema wataakikisha wanatekeleza maelekezo yaliyotolewa na serikali katika kuakikisha sekta ya elimu inaimalika ikiwemo uchumi wa  taifa.


Post a Comment

0 Comments