Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake
Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.
Tangazo hilo linawadia baada ya Bwana Trump na wasaidizi wake
wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.
Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa
Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.
Bi. Hicks alisafiri na yeye kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye
mdahalo wa Televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii.
0 Comments