Na: Vumilia Kondo
Mafunzo ya ufugaji
bora wa kuku kwa wafugaji 23 kutoka mikoa mbalimbali nchini, yamemalizika Novemba
20 katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo SUA, yakilenga kuongeza uzalishaji wa mayai na nyama pamoja na kuboresha
lishe ya jamii.
Akifunga mafunzo
hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagala ambaye ni Afisa
Tawala amesema ufugaji bora wa kuku una
mchango mkubwa katika kupunguza umasikini
Amesema watumishi
wengi na wafanyakazi wa sekta binafsi wanapaswa kupata nafasi ya kujifunza ili
hata wanapostaafu waweze kuwa na shughuli za kukuza uchumi wao na kupunguza
umaskini katika Kaya.
Naye mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE Dkt. Emmanuel Malisa amesema
mafunzo hayo yaliyodumu kwa siku nne yamehusisha nadharia na vitendo, ikiwemo
ulishaji wa vifaranga, ujenzi wa mabanda, chanjo na mbinu za biashara.
Kwa upande wake
Profea Tiisekwa Bendantungukwa kutoka AICAD amesema ufugaji wa kuku ni eneo
linaloweza kuleta matokeo ya haraka, hivyo elimu hiyo inawajengea uwezo
washiriki kuongeza kipato na usalama wa chakula majumbani.
Baadhi ya
washiriki wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kuelewa namna ya kupunguza vifo
vya kuku na kupata tija zaidi katika uzalishaji.
0 Comments