Na: Farida Mkongwe
Wanafunzi
wa Shahada ya Sayansi ya Familia na Mlaji kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) wameonesha ubunifu wao katika kubuni na kushona mavazi kupitia
maonesho ya mafunzo kwa vitendo ambayo yamelenga kuwaandaa wanafunzi hao kuingia katika soko la ajira na kujiajiri baada ya kuhitimu masomo
yao.
Naye Mhadhiri kutoka Idara hiyo, Dkt. Zahra Majili, amesema lengo kuu la maonesho hayo ni kuwapa wanafunzi fursa ya kubuni na kutengeneza mavazi yatakayowasilishwa kwa watumiaji ili kupata maoni yatakayoboresha kazi hizo.
Amefafanua kuwa shughuli hiyo ni sehemu ya tathmini ya masomo, ambapo wanafunzi hupata alama kulingana na kiwango cha ubunifu, ubora wa kazi na namna wanavyowasilisha bidhaa zao. Aidha, amewahimiza wanafunzi kutumia maarifa wanayopata chuoni katika maisha yao ya kila siku.
Amesema
wahitimu wengi wa programu hiyo tayari wamejiajiri, huku wengine wakitumia
mitandao ya kijamii kufundisha masuala ya mitindo na ubunifu wa mavazi, na
kuwashauri wanafunzi kutanguliza fikra za kujiajiri badala ya kusubiri ajira.
Wamesema
kupitia maonesho hayo wameweza kuonesha uwezo wao wa kubuni, kushona, kuchagua
vitambaa vinavyofaa na kuwasilisha bidhaa zenye ubora zinazokidhi mahitaji ya
jamii na soko la ajira.










0 Comments