Na: Adam Maruma – Morogoro.
Imeelezwa
kuwa wanawake kote nchini na duniani kwa ujumla wakipewa nafasi za uongozi
kwenye Nyanja mbalimbali wanaweza na kusaidia jamii na taifa kupata matokeo
chanya.
Hayo
yameelzwa na jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Morogoro, Mhe. Rose Eprahim wakati
akizungumza katika kilele cha siku ya wananwake duniani kwa mkoa wa Morogoro
kilichofanyika Tarafa ya Mikese kijiji cha Fulwe wilayani Morogoro.
Mhe.
Jaji Rose alisisitiza kuwa wanawake si wahanga, bali wapo katika maeneo
mbalimbali ya uongozi, uchumi na kijamii, na wanaendelea kufanya vizuri katika
majukumu yao.
Aidha,
aliwahimiza wanawake kuchangamkia fursa zilizopo katika Dira ya Taifa ya
Maendeleo ya 2050, akieleza kuwa wanawake wana jukumu kubwa katika kuifikisha
nchi kwenye maendeleo yanayokusudiwa na hivyo kuwataka kuielewa vizuri Dira ya
2050 ili waweze kuitumia kama mwongozo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo
ya taifa.
Pia
jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Morogoro aliwataka wanawake kutumia vizuri nafasi
na fursa wanazopewa na serikali kwani zimekusudiwa kuwainua kiuchumi na kijamii
na hivyo kuwakumbusha wanawake kutoacha jukumu lao la msingi la kulea watoto
katika maadili mema, kwani malezi bora ni msingi wa jamii imara.
Vilevile
aligusia changamoto ya haki ya kumiliki ardhi, akisema bado imeendelea kuwa
tatizo kwa wanawake wengi, hasa wajane, na hivyo akasisitiza umuhimu wa
kuendelea kutoa elimu ya kisheria ili kuhakikisha wanawake wanapata haki zao
ipasavyo.

0 Comments