Na: Calvin Gwabara - Dodoma
Mamlaka ya Afya ya Mimea na
Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imewezesha Tanzania kuondolewa vikwazo vya kiubora
iliyowekewa kwenye masoko mbalimbali duniani na hivyo kusaidia wakulima wa Tanzania
kunufaika na uuzaji wa mazao nje ya nchi.
Mtaalamu wa afya ya mimea kutoka TPHPA Bi. Dorah Amur akifafanua jambo kwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipotembea banda hilo. |
Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa
afya ya mimea kutoka TPHPA Bi. Dorah Amur wakati akimueleza Balozi wa Tanzania
nchini Italia Mhe. Balozi Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipotembela banda la TPHPA
kwenye maonesho ya wakulima nanenane kitaifa Jijini Dodoma kuhusu mafanikio na
jitihada zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kuhakikisha ubora wa mazao na
kufungua masoko.
“Wakulima wa wafanya biashara wa Tanzania
wamekuwa wakiuza bidhaa zao kwenye masoko mbalimbali ya kimataifa duniani
lakini kuna baadhi ya masoko yalizuia Tanzania kuingiza bidhaa zetu kutokana na
sababu mbalimbali za kiubora lakini TPHPA ikaalifanyia kazi haraka kwa kufanya
uchunguzi wa kina na kuwasilisha kwenye mamlaka za masoko hayo na kufanikiwa
kuondolewa kwa zuio hilo na sasa Tanzania inauza bidhaa hzo bila shida”
alifafanua Bi. Amuli.
Hata hivyo mtaalamu huyo amesema
pamoja na masoko ya mbali lakini pia nchi inanufaika na kuuza mazao kwenye
masoko ya afrika mashariki kwani takwimu zinaonesha Tanzania imesafirisha zaidi
zao la mchele kwenda kwenye nchi hizo kwa wingi hasa nchini Uganda, ikifuatiwa
na Kenya, Rwanda na DRC katika kipindi cha kuanzia mwaka 2024 hadi mwezi mei mwaka
2025.
“Mamla ya Afya ya mimea na viuatilifu Tanzania
inajivunia kusaidia wakulima na wafanyabishara wa Tanzania kuyafikia masoko
mbalimbali lakini pia kusaidia kuwezesha nchi kunufaika na mauzo ya bidhaa hizo
kwa kuhakikisha ubora wa bidhaa zinazosafirishwa na zile zinazoingia kukidhi
viwango vya ubora” alieleza Bi. Amuli.
Akizungumzia masuala ya
ufungashaji wa bidhaa zinazosafirishwa meneja wa Usimamizi wa afya ya Mimea na
karantini kutoka TPHPA bwana Musa Chindinda amesema kuwa hilo ni eneo muhimu
ambalo taasisi hiyo inalizingatia na kuhakikisha bidhaa zinazosafirishwa
zinakuwa katika hali ya ubora na salama.
“Sio tuu kwamba tunaangalia ubora
wa zile zinazosafirishwa lakini pia tunashirikiana na mamlaka zingine kupima na
kuhakikisha hata bidhaa zinazoingia nchini zinazingatia ubora hususani vyakula
ili kuepusha kuingiza mazao au bidhaa zenye vidudu au magonjwa hatari ambayo
yanaweza pelekea kuwekwa kwa karantini” alieleza bwana Chidinda.
Pia amemueleza Mhe. Balozi hatua
mbalimbali ambazo zinapaswa kuzingatiwa ili kupata kibali kinachoweza kuruhusu
bidhaa hizo kupokelewa na pia kutoa ushauri kwa wafanyabiashara wanaotaka kuuza
bidhaa nje ya Tanzania.
Kwa upande wake Balozi huyo wa
Tanzania nchini Italia Mhe. Balozi
Mbarouk Nassor Mbarouk amepongeza juhudi hizo kubwa zinazofanywa na TPHPA
katika kusaidia kufungua masoko ya bidhaa za Tanzania duniani na kuahidi
kuendelea kushirikiana na katika masoko mbalimbali ya mazao nchini Italia.
“Nimefurahi kuona Italia pia
bidhaa za Tanzania zinavyopata masoko duniani na kuinua uchumi wa watu na
kuingiza nchi fedha za kigeni, Hii sio kazi ndogo hasa kusaidia kuondoa mashaka
yanaywekwa na masoko kwa bidhaa za Tanzania kwakweli mnastahili pongezi na niwaombe
muendelee kusaidia nchi yetu nami kama balozi nipo tayari kushirikiana nanyi kwenye mambo yoyote
ya kimasoko nchini Italia alieleza Mhe. Balozi Mbarouk.
Mamlaka ya afya ya mimea na
viuatilifu Tanzania inashiriki maonesho ya Kilimo nanenane kitaifa jijini
Dodoma na kwenye Kanda zote kupitia ofisi za kanda za Mamlaka hiyo kote nchini.
MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA ZIARA YA BALOZI.
Meneja wa Usimamizi wa afya ya Mimea na karantini kutoka TPHPA bwana Musa Chindinda akitoa maelezo kwa Balozi. |
0 Comments