Na: Hadija Zahoro
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Idara
ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia kupitia Maabara ya Sayansi
ya Udongo imekuja na kifaa cha maabara inayobebeka (Soil Doc) ikiwa ni
teknolojia mpya inayorahisisha zoezi la upimaji wa udongo na kutoa majibu ndani
ya muda wa takriban nusu saa.
Akizungumza na SUA Media katika banda la Afya ya Mimea, Mbegu na Udongo katika viwanja vya Nanenane Kanda ya Mashariki, Mtaalam wa Maabara ya Udongo, Dominica Mbawala, amesema kifaa hicho kinaweza kupima kiwango cha phosphorus na nitrogen mahali popote.
Ameeleza kuwa wanaweza
kumpimia mkulima udongo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo katika viwanja hivyo
vya maonesho hayo na kumpatia majibu hapo hapo.
Kwa upande wake, Dkt.
Hellen Kanyagha, Mtaalam wa Afya ya Mimea, ameeleza kuwa katika maonesho hayo
ya Nanenane wapo kwa ajili ya kutoa huduma ya upimaji wa udongo, afya ya mimea
na mbegu ambapo mkulima anapata huduma hizo hapo hapo bila gharama yoyote.
“Kwa sehemu ya udongo
tumekuja na Soil Doc ambayo ina vifaa
vyote vya kisasa ambavyo vinaweza vikapima kiasi cha tindikali, potassium, nitrate na virutubisho
vingine vinavyopatikana kwenye udongo,” amesema Dkt. Kanyagha.



0 Comments