Na: Siwema Malibiche:
Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepongezwa kwa kuzalisha wataalamu
mbalimbali wenye ujuzi na weledi unaowasaidia kujiajiri katika sekta mbalimbali
na kujipatia kipato binafsi pamoja na kuchangia pato la taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa maonesho ya wakulima yanayoendelea katika Kanda ya Mashariki, mkoani Morogoro, Agosti 5, 2025, mjasiriamali kutoka SUGECO na mwanafunzi wa SUA, Bw. Ansen Ngwila, amekishukuru Chuoo hicho kwa kumuwezesha kupata ujuzi uliomwezesha kujiajiri katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kupitia SUGECO.
Pia, amesema kupitia maonesho hayo ya wakulima,
wao kama wajasiriamali husaidiwa kupata soko kwa sababu hufikiwa na wateja
wengi wanaohitaji bidhaa zao.
Kwa upande mwingine, Bw. Ngwila ametoa wito kwa
vijana na wanafunzi wengine nchini kujiingiza katika ujasiriamali ambao
utawasaidia kupata kipato cha kuendesha maisha yao badala ya kukaa na kusubiri
ajira bila kujishughulisha na kitu chochote.
Maonesho
ya wakulima ya Kanda ya Mashariki yamehusisha mikoa minne ikiwemo Morogoro,
Pwani, Tanga na Dar es Salaam, ambapo mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu
isemayo: "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,
2025."
0 Comments