Na: Mwandishi Wetu
Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Ndaki ya Kampasi ya Mizengo Pinda kimeibuka Mshindi wa Pili
katika kundi la Taasisi za Elimu
kwenye Maonesho ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika katika Viwanja
vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
Ushindi huu unaendeleza rekodi bora ya SUA katika kuonesha umahiri wake wa kutoa elimu yenye ubora wa kimataifa, kufanya tafiti zenye matokeo chanya na kuendeleza teknolojia bunifu zinazochangia maendeleo ya kilimo na kuboresha maisha ya jamii.
Kwa miaka kadhaa sasa,
SUA imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama taasisi bora nchini katika kuibua
suluhisho za changamoto za kilimo na kuongeza thamani ya uzalishaji, sambamba
na kuandaa wataalamu mahiri wa sekta hiyo muhimu.
Aidha, katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya
Mashariki yaliyofanyika mkoani Morogoro, SUA iliibuka Mshindi wa Jumla na
Mshindi wa Kwanza
katika kundi la Taasisi za Mafunzo na Utafiti,
kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo nchini.
0 Comments