SUAMEDIA

SUA yaonesha njia ya kuongeza kipato kwa kutumia mabaki ya plastiki katika kilimo

 Na: Siwema Malibiche:

Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kupitia Idara ya Mimea Vipando na Mazao ya Bustani kinaonesha namna ambavyo mkulima anaweza kubadilisha mabaki ya plastiki kama ndoo na matairi kuoteshea mboga ili jamii iweze kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro, Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka SUA Godwin Rwezaula amesema kilimo hicho ni rafiki kwa mazingira na hutumia muda mchache na eneo dogo mpaka ukuaji wake.

Aidha, amewataka wakulima kuacha kulima kwa mazoea badala yake watumie wataalamu mbalimbali wanaopatikana SUA na walio karibu na maeneo yao ili kuzalisha mazao yenye tija kwa miradi na biashara.

Aidha, ametoa rai kwa wakulima wote nchini kutumia maonesho hayo ya wakulima yanayoendelea kufanyika kupata ujuzi katika kilimo cha mboga ili kuongeza uzalishaji wa mazao yao.

Maonesho hayo ya wakulima Kanda ya Mashariki yamehusisha mikoa minne ikiwemo Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam yamebeba kauli mbiu isemayo "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, 2025".





Post a Comment

0 Comments