Na: Josephine Mallango
Mhe. Malima amefurahishwa na kilimo hicho ambacho kinatumia eneo dogo na vifaa vigumu ambavyo vimeshatumika na kuwa takataka zinazobaki baada ya matumizi badala ya kutupwa na kuchafua mazingira vifaa hivyo vinatumika kuzalishia mboga mboga kwa kutumia mbinu ya udongo kidogo huku nyingine zikitumia makapi ya vifuu vya nazi vilivyosagwa na kupata unga unaopandwa mazao .
Mkuu huyo wa Mkoa amesema wanafunzi hao wa mkondo wa Amali wanapaswa kujifunza kulima kilimo hicho cha mjini kwa vitendo kwa kuwa kitawasaidia katika matumizi madogo madogo ya kijamii ikiwemo matumizi ya mboga za nyumbani na pesa zao za kujikimu katika mambo madogo madogo ikiwemo kununua sabuni badala ya kuomba wazazi.
kwa upande wake mwanafunzi Kalunde Khamis wa kidato cha pili amesema yeye amekuwa akilima nyumbani mboga za maboga na mama yake ndiyo anamnunulia mbegu kutoka sokoni na kwamba anapenda kilimo kwa kuwa kinapunguza matumizi na kimewapa unafuu wa kupata mboga mboga badala ya kununua wanachuma nyumbani hapo hapo.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof . Raphael Chibunda amesema kwa sasa wanaangalia eneo kwa ajili ya wanafunzi hao wa sekondari kujifunza kwa vitendo ambapo kila mwanafunzi atalima mazao yake kuanzia hatua ya awali mpaka mavuno akisimamiwa na wataalamu kutoka SUA na kwamba mazao hayo yatakuwa mali ya wanafunzi wenyewe ndiyo mmiliki siyo shule wala Chuo ili iwe motisha kwa wanafunzi hao .
Wakati huo huo Mhe. Malima ametembelea maabara inayotembea ambayo imekuwa ikisaidia Serikali pindi yanapotokea magonjwa ya mlipuko ambapo amesema maabara hiyo inayotembea kwa umuhimu wake anaona zingepatikana zingine zaidi katika kila Kanda ili iwe rahisi pale inapotokea changamoto ya magonjwa iweze kutatuliwa kwa haraka.
0 Comments