Na: Siwema Malibiche
Katika kuelekea mwaka mpya wa masomo Ndaki ya Sayansi za
Jamii na Insia, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo imejipanga kupokea wanafunzi
takribani 750 katika shahada zake
3 kwa muhula wa masomo 2025/2026.
Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Samwel Kabote akizungumza kupitia SUA FM 101.1 Morogoro (Picha zote na Nicolaus Roma) |
Akizungumza katika kipindi cha Elimu na Taaluma kinachoruka kupitia SUA FM kuhusu udahili kwa wanafunzi 2025/2026, Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Samwel Kabote amesema idara hiyo inatoa shahada 3 na kuongeza kuwa Ndaki hiyo ina walimu zaidi ya 62 wenye vigezo stahiki kuhudumia wahitimu watakao wanaotarajiwa kujiunga na masomo hayo.
Amezitaja shahada
hizo ni pamoja na Maendeleo ya Jamii,
Rasilimali Watu na Sheria za kazi, na
Mipango ya Maendeleo na Usimamizi ambazo
zimelenga kuwapa uwezo wanafunzi wa kujiajiri na kuajiriwa katika taasisi
binanfsi na umma kwa kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini .
Mtangazanji wa SUA FM Adam Maruma akiendesha kipindi studio |
Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia, kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo imeanzishwa 2015 ikiwa inatoa shahada moja ambapo kwa sasa inatoa shahada mbalimbali zikiwemo shahada za umahiri na uzamivu tangu kuanzishwa kwake na imekuwa ikiongezeka kutokana na mahitaji katika soko la ajira.
0 Comments