Na: Ayoub Solomon Mwigune
Wafugaji
wa Halmashauri ya Mji Njombe wametakiwa kuchukua tahadhari mapema dhidi ya
ugonjwa wa Homa ya Kiwele ‘Mastitis’ unaoathiri Ng’ombe wa maziwa.
![]() |
Akizungumza
na wafugaji wa Halmashauri hiyo, Dkt. Benigni Temba, Mhadhiri na mtafiti wa Mradi
wa NANOCOMM, amesema Homa ya Kiwele ina aina mbili ambazo ni ile inayoonekana
kwa dalili kama uvimbe, joto na maumivu, na ile isiyo na dalili za wazi lakini
hupunguza ubora wa maziwa.
“Homa
ya Kiwele isiyo na dalili ni hatari zaidi kwa sababu haionekani kwa macho,
hivyo vipimo vya maabara ni muhimu kwa utambuzi sahihi. matibabu yanapaswa
kufanyika mapema na dozi za dawa kukamilishwa,” amesema Dkt. Temba.
Naye
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji Njombe, Bi. Frida Mlowe, amewashukuru
wataalamu wa SUA kwa kutoa mafunzo na kufanya uchunguzi wa ugonjwa huo katika
halmashauri hiyo. Amesema elimu iliyotolewa itasaidia wafugaji kudhibiti homa
ya kiwele kwa ufanisi.
![]() |
Wafugaji
waliopata mafunzo, Fedrick Gaspa na Ally Kitogela, wamesema kuwa elimu
waliyoipata imesaidia kuelewa changamoto za ugonjwa huo na hatua za
kuchukua ili kuboresha uzalishaji wa maziwa na kuongeza kipato.
Mradi
wa NANOCOMM unatekelezwa katika mikoa ya Tanga, Iringa, Mbeya, Njombe na
Arusha. Tafiti zinazofanywa zinawalenga wafugaji kubaini vyanzo vya homa ya
kiwele na kutafuta tiba mbadala za kuudhibiti ugonjwa huo nchini.
0 Comments