Na: Siwema Malibiche
Wananchi
Mkoani Morogoro wametakiwa kuilinda misitu ya hifadhi kwa kuepuka kufanya
uharibifu kutokanao na shughuli za kibinadamu
ikiwemo ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya maandalizi ya mashamba ili
kutunza uoto wa asili.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bw. Mussa Kilakala akipanda mti katika Msitu wa Hifadhi wa Kimboza (Picha zote na Nickolous Roman) |
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya
Morogoro Bw. Mussa Kilakala wakati akizindua Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira Asilia
Hifadhi za Misitu ya Kimboza na Ruvu
ambapo zoezi la upandaji wa miti katika huo litasaidia kuboresha vyanzo vya maji.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine
Cha Kilimo SUA, Dkt. Charles Kilawe, ambae pia ni Mkuu wa Mradi amesema kuwa jukumu
lao kama mradi ni kuoteasha miti sehemu ilizoharibiwa kwa lengo kuendelea
kutunza uoto wa asili.
![]() |
Mkuu wa Mradi Dkt. Charles Kilawe (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bw. Kilakala (katikati) wakitete jambo |
Dr.
Kilawe ameongeza kuwa miti mingi ya asili hupotea katika misitu nchini kwa sababu ya uwepo wa mimea vamizi mfano Misedelea
ambayo kitaalamu hushauriwa kupandwa mbali na hifadhi ya misitu huku akitambua umuhimu wa misitu kwa jamii
husika ikiwemo upatikanaji wa dawa za
asili.
Kwa
upande wao, Wanafunzi wa Shahada ya
Awali ya Sayansi ya Misitu kutoka SUA Bw.
Charles Malendeja na Bi, Miriam Mwashoma wamewataka wanafunzi kuwa na tabia ya
kupanda miti katika mazingira ya
nyumbani na misitu huku wakitambua kuwa
misitu inafaida kubwa kwa jamii.
Naye, Mhifadhi Mwandamizi wa Misitu Wilaya ya Morogoro Bw. Stanley Kweka amempongeza
Dkt. Charles Kilawe kutoka SUA kwa kuja na mradi utakaoisaidia jamii kurejesha
miti ya asili ambayo inapotea huku
akitambua kuwa uwepo wa ushirikishwaji
thabiti wa jamii katika utunzaji wa
misitu Mkoani Morogoro
![]() |
Katika uzinduzi huo wanafunzi
kutoka wa Shahada ya Awali ya Sayansi ya Misitu
zaidi ya 180 kutoka SUA wameshiriki katika upandaji wa miti takriban 20,000 kwa kushirikiana na
wanakijiji na wadau mbalimbali wa Mazingira na misitu kwa ujumla.
Mradi huo unadhaminiwa na Programu ya Ruzuku Ndogo za Mfuko wa Mazingira Duniani (The Global Environment Facility Small Grants Programme (GEF SGP) na unatekelezwa kwa pamoja na Shirika la Uhifadhi Mazingira kwa Jamii na Wanyamapori (ECOWICE), Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na unasimamiwa na Dr. Charles Kilawe.
Picha chini ni matukio mbalimbali katika upandaji wa miti
0 Comments