Arusha
Waziri wa Mifugo, na Uvuvi, Mhe. Abdalah Ulega amewataka madaktari wa wanyama nchini kutumia taaluma yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kudhibiti makanjanja ambao wamekuwa wakiuza dawa feki na kuleta athari kubwa kwenye Mifugo.
Waziri wa Mifugo, na Uvuvi, Mhe. Abdalah Ulega (aliyeshika chupa)akikagua bidhaa katika mkutano huo
Mhe. Ulega ameyasema hayo leo jijini Arusha kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kongamano la 42 la Chama cha Kitaaluma cha Madaktari wa Wanyama Nchini,TVA lililofanyika katika hotel maarufu ya Ngurdoto iliyopo Arusha.
Ulega amesema kuwa,amesikia ombi lililotolewa na viongozi wao kuhusu serikali.kuajiri madaktari wasaidizi katika maeneo mbalimbali kwani waliopo hawatoshi ili.waweze kutoa huduma hiyo hadi maeneo ya vijijini na kuwa changamoto hiyo itafanyiwa kazi .
"Ombi lenu nimelisikia kuhusu kuajiri madaktari wengi ambao watasambaa katika maeneo mbalimbali.ya nchi ili huduma iweze kutolewa kwa urahisi kwa.wananchi,na ombi hilo nitalifikisha kwa Rais Samia kama mlivyoniomba."amesema Ulega .
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa mkutano
Aidha amesema kuwa, serikali imetenga shilingi Bilioni 460 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kuongeza thamani ya biashara ya mifugo nje ya nchi ambapo kati ya hizo bilioni 28.1 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa chanjo ya mifugo nchini.
Waziri wa Mifugo, na Uvuvi, Mhe. Abdalah Ulega (aliyekaa katikati) akiwa na baadhi ya washiriki wa mkutano huo (kulia ni waliokaa) ni Mwenyekiti wa TVA Prof. Hesron Karimuribo
Ulega amesema kuwa katika ukuaji wa uchumi pamoja na afya bora kwenye jamii kwa miaka ya hivi karibuni imebainishwa kuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yatokayo kwa wanyama na kuja kwa binadamu.
"Kulingana na umuhimu huo Serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hiyo ili kutokomeza kabisa changamoto hiyo na kuendelea kukuza uchumi wa nchi yetu."amesema Ulega .
Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Esron Karimuribo amemshukuru Waziri kwa kuja kufungua mkutano huo kwani ameonesha mapenzi mema na chama hicho .
Prof.Esron amesema kuwa ,malengo ya kuzungumza namna ya kutokomeza magonjwa ya Mifugo ili kuongeza tija ya uzalishaji huku malengo mengine ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara ya mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya wadau wa sekta ya mifugo wakizungumzia umuhimu wa kongamano hilo ,Salim Msellem kutoka Kampuni ya Farmers Centre /Farmbase amesema kuwa,amemshukuru Rais Samia kwa kutengeneza mazingira mazuri ya wataalamu wa Mifugo ambao watahakikisha sekta hiyo inakuwa kwa kasi.
"Tunaiomba serikali tuendelee kushirikiana ili kufanikisha usafirishaji wa mazao ya Mifugo nje ya nchi na sisi tuna ahidi kuendelea kushirikiana zaidi katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa."amesema Salim.
Aidha amesema kuwa, kampuni hiyo imetimiza miaka 30 ya kutoa huduma yenye ubora wa hali ya juu kama zilivyo sawa kutoka Ulaya .
0 Comments