Na:
George Joseph
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) kupitia Taasisi ya Elimu ya kujiendeleza (ICE) kimeandaa mafunzo ya ufugaji
bora wa Samaki utakao husisha wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini ili
kujifunza namna bora ya kufuga Samaki kitaalamu.
Akifungua mafunzo hayo ya siku
tatu yaliyoanza tarehe 3 Disemba 2024 ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya
Kujiendeleza Dkt Devotha Mosha amesema kuwa mafunzo yatagawanyika katika sehemu
mbili darasani kwa nadharia kisha wafugaji watajifunza kwa vitendo na kutembelea
eneo la mabwawa ya kufugia Samaki chuoni hapo.
Aidha ameeleza kuwa SUA imeandaa
mafunzo hayo kwa lengo la kuwezesha wafugaji kufuga kwa kuzingatia taratibu
zote za ufugaji kuanzia kuandaa mabwawa mpaka wakati wa uvunaji na kutaka
washiriki hao wawe mfano mzuri katika sekta ya ufugaji wa Samaki nchini.
Pichani ni washiriki katika mafunzo ya ufugaji wa Samaki wakiwa katika mafunzo kwa vitendo. |
Dkt Devotha pia ameongeza kuwa Samaki
ni kitoweo muhimu sana na pia ni chanzo cha mapato hivyo wafugaji wakipata
elimu juu ya ufugaji bora itawawezesha kukuza vipato vyao na kunyanyuka
kimaisha.
Aidha washiriki wa mafunzo hayo
wamesema kuwa wanategemea kujifunza mengi zaidi wawapo chuoni kwani SUA
inasifika nchini kuwa Chuo bora kwenye upande wa kilimo na ufugaji.
Mafunzo hayo ya siku tatu yameanza tarehe 03 Disemba mpaka tarehe 06 disemba 2024 yanashirikisha washiriki zaidi ya 10 kutoka mikoa mbalimbali nchini na yanahusisha wataalam pamoja na wahadhiri mbalimbali kutoa SUA.
0 Comments