Na: Siwema Malibiche
Kitengo cha Ugani kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE
kimeendesha mafunzo kwa idara mbalimbali
ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ili kuongeza uelewa zaidi katika shughuli za
ugani ili kuleta maendeleo kwa taifa
kupitia sekta ya kilimo.
Mkuu wa Kitengo cha Ugani kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE – SUA Dkt. Emmanuel Malisa (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa ICE Dkt. Devotha Mosha alitevaa miwani wakiwa katika warsha |
Akizungumza wakati wa
warsha hiyo iliofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya
Edward Moringe mkoani Morogoro Mkuu wa Kitengo cha
Ugani kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE – SUA Dkt. Emmanuel Malisa amesema wamekuja na warsha hiyo kwa idara ili kutoa
mafunzo juu ya ugani lengo likiwa ni
kukuza na kuboresha shughuli za ugani kwa kuleta utaratibu bunifu utakaosaidia
kuratibu vizuri shughuli zake ndani ya SUA
Aidha, amesema wamekuja
na warsha hiyo kufuatiwa na kuwepo kwa baadhi ya changamoto za kiutendaji katika idara mbalimbali ikiwemo
ucheleweshwaji wa taarifa mbalimbali za maeneo ambayo zimefanyika shughuli za
ugani na anaamini kuwa warsha hiyo italeta msukumo mpya baada ya mapendekezo na
boresha shughuli za ugani kwa kuleta utaratibu bunifu ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo .
Kwa upande wake, Mhadhiri,
kutoka Idara ya Mimea Vipando na Kilimo cha Bustani na Mwenyekiti wa kamati ya Ugani katika Ndaki ya Kilimo Dkt. Yasinta Zogela
amesema amejifunza mengi kupitia warsha hiyo ambayo itaenda kuboresha na
kuwaelimisha wafanyakazi wengine na anamini itasaidia kwenye uboreshaji wa taarifa muhimu ambazo
zinahitajika kwenye hatua mbalimbali za kiutawala wa chuo na kusambaza huduma
za kiugani kwa wepesi na weledi katika
jamii inayowazunguka.
Naye, Afisa Maktaba Mkuu katika Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya Kilimo Jabir Jabir amesema kupitia warsha hiyo itasaidia kuboresha namna ya kutoa elimu thabiti ili kuwafikia wakulima wengi kupitia “Mkulima Collection yenye malengo ya kuwasaidia wakulima kupata taarifa mbalimbali za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambapo wakulima watapata taarifa za machapisho mbalimbali yatakayowasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi.
Mafunzo hayo yaliyofanyika
katika ukumbi wa ICE ndani Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo yameudhuliwa
na wajumbe zaidi ya 20 kutoka katika Ndaki, Kurugenzi na Idara mbalimbali za
chuo ambapo ikiwa na maratarajio ya kuwaunganisha wataalam kutoka SUA na jamii
kwa kutoa elimu itakayosaidia kutatua changamoto zinazowakabili wakulima kwa
maslahi ya Taifa.
0 Comments