SUAMEDIA

Serikali imeendelea kuwekeza kwenye teknolojia na tafiti ili kukuza kilimo

Serikali imeendelea kuweka kipaumbele kwenye kukuza kilimo nchini ikiwemo kuwekeza kwenye teknolojia, tafiti pamoja na kuongeza vifaa vya kuboresha kilimo kwa wakulima. 


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Husein  Omar (anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula) wakati akizungumza katika kongamano la Miaka 63 ya Uhuru lililoandaliwa na TBC kwa kushirikiana na SUA Desemba 06, 2024.

Omar ameyasema hayo wakati akiongea katika mada ya kuangalia maono ya Serikali katika kilimo kwa kuangalia sehemu tulipotoka, tulipo na tunapoenda.

"Tumeimarisha huduma za kiugani,  wizara imetoa magari 29 kwa mikoa na halmashauri na matrekta 500, vishikwambi 5426 kwa ajili ya kukusanya data za kilimo,  pikipiki 6444 na tunaendelea kutoa pembejeo za ruzuku ili kukuza sekta ya kilimo", alisema Omar.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na SUA katika kupata wataalamu (wanafunzi) bobezi katika sekta ya kilimo watakaotumika kutekeleza mpango wa programu ya BBT.


Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo  - Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala amewashukuru TBC kwa kutambua mchango wa Chuo, akisema uwepo wa kongamano hilo utaenda kuamsha hali ya kujituma kwa wanafunzi zaidi kupitia mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT).

Mhadhiri wa Idara ya Mimea, Vipando na Mazao ya Bustani wa Chuo Kikuu cha Sokoune cha Kilimo (SUA), Dkt. Yasinta Nzogela wakati akitoa mada kuhusiana na kilimo cha kisasa, ushiriki wa vijana na mageuzi ya uchumi wakati wa kongamano hilo amesema Tanzania inazalisha chakula kwa asilimia 120 tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma jambo ambalo linatakiwa kuungwa mkono





Post a Comment

0 Comments