SUAMEDIA

Wanafunzi wa SUA wakubalika zaidi katika Soko la Ajira

Na: Tatyana Celestine

Matokeo ya Mabadiliko ya Mitaala yanayofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) yamewezesha Chuo hicho kuwa bora zaidi katika kutoa mafunzo yenye tija pia kwa vitendo yanayopelekea kupata ajira kwa haraka inayotokana na kuchagua na kufundisha masomo yanayoweza kumfanya mwanafunzi kujiajiri hata kupata wepesi katika ushindani wa Soko la Ajira.

                        

Zoezi la kufanya Tathmini  kupitia Mjadala wa Uzoefu juu ya Mafunzo kwa Vitendo Shahada ya Usimamizi wa Utalii 2024 Idara ya Utalii na Mapumziko Huishi SUA umeibua mambo muhimu ambayo yamesaidia kuweza kuona mafanikio katika utoaji wa elimu na ufatiliaji wa wanafunzi kwenye mafunzo kwa vitendo kwa lengo la kuendelea kuboresha elimu itolewayo chuoni hapo.

                    

Akizungumza mara baada ya Mjadala huo Profesa Mshiriki kutoka Idara ya Utalii na Mapumziko Huishi SUA, John Mgonja ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mjadala huo amesema wanafunzi wa SUA wanaajirika zaidi kulinganisha na vyuo vingine kutokana na heshima ya kazi, kujituma, uwezo wa kutafsiri walichofundishwa na kukiweka katika vitendo hiyo ni sababu SUA inatoa fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo kwa miaka mitatu.

                                     

Alipotakiwa kuzungumzia umuhimu wa kuchagua mafunzo yanayohusiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa mwanafunzi Prof. Mgonja amesema kupitia mabadiliko ya mitaala wameweza kuona vitu muhimu ambavyo vinamjenga mwanafunzi kujiandaa kwenye ajira na kuwasikiliza waajiri nini wanataka hivyo chuo kimechagua masomo muhimu ili wanafunzi wapate kufahamu kulingana na mahitaji ya soko ikiwemo sehemu ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwani ni kozi nzuri inayomjenga mwanafunzi kuwa salama katika sehemu ya kazi.

                  

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Idara ya Utalii na Mafunzo Uhishi SUA, Ernest Mwamwaja amesema kupitia mafunzo kwa vitendo wanafunzi kutoka SUA wamejitofautisha na wengine kutokana na ubora wao wa kuonesha ubunifu ambao amewahahakikishia wazazi, walezi kuwa mwanafunzi anaposoma Kozi ya Utalii na Mapumziko Huishi kwa miaka mitatu atakuwa na uwezo wa kufanya kazi zake kwa kiwango cha juu.

                    

Naye Mjumbe kutoka Idara ya Uhandisi Misitu na Sayansi za Mazao ya Misitu Mbonea Mweta amesema semina hizi zimekuwa sehemu ya kupata masuluhisho ya changamoto baada ya kujifunza na hiyo imeonekana mara baada ya kumaliza semina hiyo na kuona kuwa SUA iko vizuri kwa upande wa wanafunzi wake wanapokuwa katika mafunzo kwa vitendo hivyo jukumu walilonalo kwa sasa ni kujitangaza watu waone shughuli zinazofanywa na wanafunzi kutoka chuoni hapo.

 


















PICHA ZAIDI BOFYA LINK HAPA CHINI

Post a Comment

0 Comments