SUAMEDIA

Vijana 300 kutoka SUA wategemewa kujikwamua kiuchumi kupitia ufugaji wa Kuku kila mwaka

Na: Tatyana Celestine

Katika kuhakikisha Vijana wanaosoma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na maeneo jirani wanaweza kujikwamua kiuchumi na kujifunza kwa vitendo kupitia ufugaji wa Kuku, Chuo hicho kinaingia makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya AKM Gritters CO LTD ambapo kwa pamoja wanategemea kuwakwamua vijana wapatao 300 kila mwaka.

                             


Akizungumza wakati wa kuwasilisha wasilisho lake, Mkurugenzi wa Kampuni ya AKM Gritters CO LTD Bi. Elizabeth Swai amesema Kampuni yao imeweza kusaidia vijana wengi mkoani Tanga hivyo wameona ni wakati sahihi sasa Tanzania kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA kuanza kufaidika na fursa hilo kwani kushirikiana kwao kutasaidia kutoa elimu ya masoko, ujasiliamali, teknolojia mpya, menejimenti pamoja na kujitegemea kwa vijana hao kwa kutumia eneo dogo kufuga kuku na kupata faida.                                          

Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda ameunga mkono ushirikiano huo na kuomba kampuni hiyo kuharakisha nyaraka za mashirikiano hayo ili kuyafanyia kazi  kuhakikisha jambo hilo linafanyika kwa haraka kwani SUA kupitia wao itafaidika sio tu kwa wanafunzi kujifunza lakini pia kuhakikisha wanapata elimu ya kujikwamua kiuchumi kutokana na mafunzo hayo hivyo SUA itakuwa tayari kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi kutekelezea shughuli hizo.

                            

“Mhe Rais amezitaka Taasisi za Umma zianze kufikiria katika kilimo na imetokana na experience mbaya ya Kiwanda cha Sukari… kwa hiyo sisi kama tunapata patna tukafikiria module inayoweza kuwa na pande mbili mafunzo na wengine wasio na eneo nyumbani wapate mahali pa kujifunzia hapohapo kwenye kituo” amesema Prof. Chibunda.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kutoka SUA, Dkt. Felix Nandonde ameelezea mradi huo anavyouelewewa na kusema kuwa mradi una umuhimu kwa Chuo kutokana na kusaidia vijana na Wanawake katika ufugaji kuku, kupata mikopo ya kukuzia biashara zao na kuwafuatilia kwa ukaribu hivyo kushirikiana na SUA ni nafasi kwao kujitanua kwani chuo hicho kinaweza kuchangia maarifa waliyokuwa nayo, ardhi pamoja na vijana wenye hari ya kuzalisha na kuinua tasnia ya kuku.

                              

Alipotakiwa kuelezea ni kwa namna gani zoezi hilo litakuwa na faida kwa Chuo Mtaalamu wa Kuku kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw. Said Mbaga amesema mradi huo  umekuja SUA kwa wakati sahihi kwani utasaidia nyakati ambapo wanafunzi hawapo kuweza kushughulika na biashara ya kuku tofauti na sasa eneo linalotumika kwa kufugia kuku limekuwa maalum kwa ajili ya kufanyia Tafiti pekee.

                        

                                

Bw. Mbaga ameongeza kuwa wanafunzi wengi wamekuwa na uelewa wa awali katika ufugaji wa kuku na kukosa elimu ya biashara, masoko na ujasiliamali katika nyanja hiyo hivyo kuku wanapokuwa wengi kama mfugaji anatakiwa kujua mahitaji, soko na bei pamoja na kuweka kumbukumbu kulingana na wakati hivyo kupitia zoezi hilo litamfanya mwanafunzi aliyesoma darasani aweze kupata mafunzo kwa vitendo kwa kufuga kuku kibiashara kwa kutambua lugha nzuri ya kutumia, mikopo inapatikanaje, pamoja na masoko yaliko.







                                







Post a Comment

0 Comments