Na: Siwema Malibiche
Wananchi mkoani Morogoro na mikoa
ya jirani wameaswa kutembelea katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kujifunza
mambo mbalimbali yaliyomo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa maslahi
yao na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa Agosti 4,
2024 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander
Manyeti mara baada ya kumaliza kutembelea mabanda mbalimbali yaliyopo katika
viwanja hivyo huku akisisiza kuwa maonesho
hayo yanatoa wigo mpana kwa wakulima kujifunza
na kubadili mifumo yao ya kilimo, ufugaji na uvuvi kwa maendeleo ya
Taifa.
Amesema ameona jinsi ambavyo
sekta binafsi wanaipenda nchi yao kwa sababu pamoja na kufanya kazi zao
kibiashara wanatoa huduma kwa sehemu kubwa za kuwasaidia wafugaji, wavuvi na
wakulima
Vile vile Mhe. Mnyeti amesema kuwa kazi ya Serikali ni kuonesha njia, kusimamia
na kuonesha mwelekeo katika sekta ya kilimo hivyo ni vizuri kwa taasisi za
serikali kuwa mfano kwenye aina ya bidhaa wanazopeleka kwenye maonesho hayo kwa
kuzingatia ubora wa bidhaa hizo.
Pia, amefurahishwa na aina ya teknolojia zilizooneshwa na wadau mbalimbali wa kilimo wanaoshiriki kwenye Maonesho hayo pamoja na halmashauri ambazo zitaendelea kukuza uchumi wa taifa na kuunga mkono jitihada za Rais wa Samia Suluhu Hassan.
Aidha Mhe. Mnyeti amezitaka taasisi husika kuendelea kutoa
elimu kwa jamii ili kukuza uchumi na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira ikiwemo misitu
kwa kuepuka kufanya matendo yatakayo haribu mazingira kwa kufuata sheria zilizowekwa
ili kulinda uoto wa asili.
0 Comments