Na, Winfrida Nicolaus
Imeelezwa kuwa Mafunzo kwa Vitendo pamoja na Tafiti zenye tija
katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo SUA kwa lengo la kumuwezesha kijana kuajirika na kujiajiri mwenyewe
inaleta hamasa kubwa kwa watu walio wengi hasa vijana kutafuta fursa kwenye
Sekta hiyo.
Hayo yamebanishwa na Mwalimu Emmanuel Mwakalibule kutoka Shule
ya Upendo Amani iliyopo Kihonda Mtaa wa Kiegea A Manispaa ya Morogoro wakati
alipotembelea Banda la SUA kwenye Maonesho ya Nane Nane Kanda ya
Mashariki katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mkoani
Morogoro yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora wa Serikali
za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Amesema maisha ya watanzania wengi yanategemea kilimo
hivyo ni vyema kuwaelekeza vijana kwa vitendo waone na kutambua fursa
mbalimbali zilizopo kwenye Sekta hiyo ili iwe chachu ya wao kuona umuhimu wa kilimo kwenye maisha yao na kukitumia kama fursa katika kuleta maendeleo yao
binafsi na nchi kwa ujumla.
Mwalimu Emmanuel amesema wanafunzi wao wamejifunza katika Banda la SUA ni
zaidi ya matarajio yao kwakuwa wameona pia namna Sayansi ilivyo muhimu na namna
ilivyo msaada kwa jamii hivyo wanauhakika wanafunzi wao wameelewa na kupata
hamasa ya kujiunga na Chuo hicho na hilo ndilo wanalohitaji kwakuwa kilimo kina
fursa nyingi zaidi inaonesha wazi elimu inayotolewa SUA itawapeleka moja kwa
moja kwenye soko la ajira .
“SUA ni Chuo kikubwa kutokana na ubora wa kozi pamoja na
Taaluma wanayoitoa imeleta chachu kubwa kwetu kutembelea Banda lao hata
hivyo sisi kama walimu tumeangalia hali ya sasa ya soko la ajira lilivyo na
mambo mengine yanayoendelea lakini pia Serikali inasisitiza kuwafundisha watoto
elimu itakayowawezesha kujiajiri wao wenyewe na SUA ni mfano ulipo hai wa
utoaji wa elimu hiyo”, amesema Mwalimu Emmanuel
Kwa upande wake Mwanafunzi Ashrafu Juma amesema amevutiwa sana
na mafunzo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayotolewa na SUA kwa kuwa yanaonesha
uhalisia wa nini Chuo hicho kinafanya kwa wakulima na kwamba amefurahishwa
zaidi kuona uzalishaji wa Vifaranga vya samaki, ufugaji wake na mavuno yake kwa
tija na kuelewa kuwa Kilimo kina faida kubwa endapo utakifanya Kitaalam.
Naye Erica Kimambo amesema amajifunza na kujionea shughuli
mbalimbali zinazofamywa na SUA ikiwemo namna ya kufuga, kulima kilimo chenye
tija lakini pia kuona bidhaa mbalimbali zitokanazo na kilimo hivyo
imempa hamasa ya kujiunga na Chuo hicho kwakuwa atapata elimu kwa vitendo
itakayomuwezesha kutotegemea kuajiriwa pekee bali kuweza kujiajiri mwenyewe.
“Niseme niwaombe wanafunzi wenzangu kutoka shule zingine
kuweza kuja kwenye maonesho haya katika Banda la SUA kujifunza kwa kuona kwa
macho fursa zilizopo kwenye Kilimo, ufugaji na uvuvi lakini pia kupata elimu
ambayo itawasaidia kuchagua fani zenye manifaa kwao”, amesema Erica Kimambo
0 Comments