Na, Winfrida Nicolaus
Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Idara ya Sayansi ya Lishe na Stadi
za Mlaji Kitengo cha Ushonaji watoa mafunzo ya Bunifu mbalimbali ikiwemo kuviongezea
thamani vitu vilivyopo kwenye jamii ambayo yanamuwezesha Muhitimu kuweza kupata
fursa ya kujiajiri mwenyewe.
Hayo
yameelezwa Agosti 4, 2024 na Dkt. Zahra Majiri Mhathiri SUA wakati akizungumzia
bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na wanafunzi wanaosoma kozi hizo katika
Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu kama Nanenane Kanda ya
Mashariki yanayoendelea mjini Morogoro
Amesema
katika maonesho hayo wameleta bidhaa mbalimbali ambazo zimebuniwa na kutengenezwa
na wanafunzi wa kozi hiyo ambapo inaonesha jinsi wanafunzi hao walivyoongezea
thamani vitu mbalimbali yakiwemo mapipa yaliyotumika na kugeuzwa meza na viti ambayo
vinaweza kuwekwa kwenye bustani (garden), baa na hata kwenye migahawa hivyo wanayauza
na kujiingizia kipato.
“ Kama
unavyoona hizi bidhaa zilizopo hapa haya yalikuwa ni mapipa tumetumia kama
malighafi, haya mapipa mwanzoni yalikuwa yameshatumika lakini baada ya kutumika
yanakuwa hayana kazi sasa ili yasiwe taka yakaongezewa thamani wakabuni kwa
kuyakata katika miundo tofauti na kutengeneza meza na viti kama unayoyaona”, amesema Dkt. Zahra Majiri
Dkt .
Zahra Majiri ameongeza kuwa wanazo bidhaa nyingine ambazo wanafunzi haohao
wamezitengeneza ikiwemo batiki zilizotengenezwa kwa kufuata viwango vyenye ubora kwakuwa
azipauki wala kuchakaa haraka na kuna zile bidhaa zilizotengenezwa kwa mikono
kwa kutumia nyuzi za aina mbalimbali na bidhaa hizo zinawakilisha utamaduni wa
asili za kitanzania.
Amesema
bidhaa zao ni tofauti na za watu wengine kwakuwa zimtengenezwa kwa viwango
vyenye ubora unatakiwa na kuzingatia uhifadhi hivyo vinaishi kwakuwa
vimetengenezwa kwa usahihi.
0 Comments