Na: Calvin Gwabara - Dodoma.
Serikali yakipongeza Chama cha
Maafisa ugani Tanzania (TSAEE) kwa kazi nzuri inayofanywa na wagani hao nchi
nzima katika kusaidia wakulima,wafugaji na wavuvi kuzalisha kwa tija na
kupelekea nchi kujitosheleza kwa chakula hasa nafaka.
1.
Mratibu
wa Sekta ya Mifugo na Uvuvi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bw. Wilson Shimo wakati
akifunga Kongamano la maafisa ugani nchini lililoandaliwa na (TSAEE).
Pongezi hizo zimetolewa jijini
Dodoma na Mratibu wa Sekta ya Mifugo na Uvuvi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Bw.
Wilson Shimo wakati akifunga Kongamano la maafisa ugani nchini lililoandaliwa
na (TSAEE) na kuwakutanisha wagani
katika sekta ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi kutoka nchi nzima ili kujifunza teknolojia
mbalimbali mpya zinazooneshwa mwaka huu kwenye maonesho ya Kilimo Nanenane kitaifa.
“Nitumie nafasi hii kuwapongeza
na kuwashukuru kwa niaba ya Serikali kwa kazi nzuri na kubwa mnayoifanya ya
kutumia utaalamu wenu kutoa ushauri wa kitaalamu kwa jamii kwenye sekta zote
tatu za Kilimo,Mifugo na Uvuvi kuweza kuongeza tija na kupelekea utoshelevu wa
chakula katika nchi yetu hususani katika Kilimo cha nafaka na ndio maana
serikali inaendelea kuboresha mazingira yenu ya kazi ili mfanye kazi vizuri
zaidi”alisema Bw. Shimo.
Aliongeza “Kwa kutambua mchango
wenu na kuboresha mazingira yenu ya utoaji huduma Serikali imenunua magari 15, Pikipiki
kwa maafisa ugani nchi nzima, Vishikwambi 4305, Vifaa vya kupima udongo na
ujenzi wa nyumba 50 za maafisa ugani kwenye ngazi za kata unaendelea, hii ni
sehemu tu ya mengi ambayo Serikali inayafanya katika kuboresha utendaji wenu na
kutatua changamoto zinazowakabili ili kuchochea ufanisi hivyo juhudi hizo za
serikali ziwafanye muendelee kuwajibika kwenye maeneo yenu”.
Amesema jukumu la kuwapatia
maafisa ugani mafunzo rejea sambamba na vitendea kazi ni la wizara zote za
Kisekta kwa kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI hivyo ni muhimu kuendelea
kukumbushana katika umoja huo na kupitia kwa Chama chao ili wataalamu hao ili
kupunguza changamoto zinazowakabili kama sio kuzimaliza kabisa.
Amesema hadi sasa Tanzania kuna
maafisa kilimo ugani 7000 kwa upande wa kilimo, Mifugo wapo 3642 na Uvuvi wapo
647 na kwa takwimu hizo inaonesha kuwa idadi hiyo bado ni ndogo ikilinganishwa
na maeneo yaliyopo kwani zipo kata 3659,vijiji 12,319,Mitaa 4,233 na haya yote
yanahitaji kuwa na wagani lakini pamoja na uchache wao lakini wanatoa huduma
nzuri kukidhi mahitaji.
Nae kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama cha Wagani Tanzania (TSAEE) Prof. Catherine Msuya kutoka Chuo Kikuu ch
Sokoine cha Kilimo (SUA) amesema chama hicho kimeanzishwa mahususi kwa lengo la
kuwakutanisha wagani kwa pamoja, kubadilishana uzoefu na kubuni mbinu za pamoja
za kusaidia utoaji wao wa huduma kwa jamii ili kusaidia kuongeza tija na kuinua
uchumi wa Taifa.
1. Mwenyekiti wa Chama cha Wagani Tanzania (TSAEE) Prof. Catherine Msuya na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu ch Sokoine cha Kilimo (SUA) akieleza malengo ya Kongamano hilo.
“Tunafarijika sana kama chama
kuona serikali inatambua mchango wetu kama maafisa ugani katika kuifanya nchi
kujitosheleza kwa chakula kwa kipindi kirefu,pia tunamshukuru sana Rais wa
Serikali ya Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wagani na
kuboresha mazingira yao ya kazi katika kutoa huduma kwa kuwanunulia wagani
Pikipiki nchi nzima na vifaa vingine ikiwemo vya kupima udongo na mengine mengi
anayoyafanya kwakweli anatutia moyo sana na kuongeza ari ya wagani katika kutoa
huduma bora zaidi” alieleza Mwenyekiti wa TSAEE Prof. Catherine .
Amesema mwaka huu wamekutana
kwenye kongamano la Chama chao wakati wa Maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma ili
kujifunza teknolojia na mbinu mbalimbali zinazooneshwa kwenye maonesho hayo ya
kitaifa na kujadiliana namna ya kuzipeleka kwa wakulima kwenye maeneo
wanayotoka na kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alilolitoa mwaka
jana kwenye mkuatano wao wa mwaka.
Prof. Catherine amesema Chama
hicho kitaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine wa maendeleo katika
kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo maafisa ugani hao kwenye
utoaji wa huduma kwa jamii ikiwemo mafunzo rejea ili waweze kupata taarifa mpya
na tenkolojia mbalimbali za kisasa zinazozalishwa.
TSAEE imewakutanisha maafisa
ugani kutoka nchi nzima kwenye maonesho hayo ya Nanenane kitaifa yanayofanyika
Jijini Dodoma kwenye Kongamano la siku tatu na kujionea na kujifunza teknolojia
mbalimbali zinazooneshwa mwaka huu pamoja na kupata uzoefu kutoka kwa wataalamu
kutoka Marekani na China walioshiriki kongamano hilo.
1.
Prof.
Dismas Mwaseba kutoa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA akitoa uzoefu wake
na mchango wake kwenye kongamano hilo.
1. Prof. Carol Smathers kutoka Chuo Kikuu cha Ohio nchini Marekani ambaye ni mdau wa TSAEE akieleza uzoefu wake wa matumizi ya Ugani kwenye kuwezesha kilimo na nafasi Umuhimu wa Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika kujifunza kilimo.
0 Comments