Na: Tatyana Celestine
Menejimenti ya Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA) inastahili kupogezwa kwa kuwa tofauti na mahala
pengine kwa kuona umuhimu wa Mafunzo ya Afya ya Akili kwa wafanyakazi wote wa
Kampasi za SUA na kuhakikisha wanapata uelewa wa kutosha ili kukabiliana na changamoto zinazoweza
kujiokeza wakiwa kazini na kijamii kwa ujumla.
Amesema hayo ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo ya Afya ya Akili yaliyofanyika katika Kampasi ya Solomoni Mahlangu Mjini Morogoro Daktari Bingwa wa Figo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Garvin Kweka na kufanya wafanyakazi wa Chuo hicho wote kupata fursa ya kujifunza kama matarajio ya Menejimenti ya chuo hicho ilivyotarajia.
Aidha ameomba Menejimenti ya SUA
kuona umuhimu wa kuweka eneo maalumu chuoni hapo ambalo litamsaidia mfanyakazi
kusikilizwa anapokutana na changamoto za kihisia, kimwili, jamii ,dini na akili
kutokana na uhalisia wa matatizo ya namna hiyo kuongezeka kwa kiasi kubwa
nyakati za sasa nchini kutofautisha na zamani hivyo kwa kutumia muda wa
kujifunza mara kwa mara na ukaribu utasaidia kupunguza madhara yatokanayo na
tatizo la Afya ya akili.
Daktari huyo amebainisha kuwa watu wengi wanatafuta akili za darasani zaidi intelligence quotient (IQ) na kusahau akili hisia Emotional intelligence (EQ) ambapo ni chanzo cha kuharibu kila kitu katika safari ya kutafuta mafanikio kwa mwanadamu hivyo ili waweze kufanikiwa wanatakiwa kuzingatia vyote kwa pamoja nayo itawafanya wasijitenge na jamii zaidi kuweza kutumia fursa mbalimbali hata kugeuza matatizo kuwa fursa na kuachana na msongo wa mawazo ambao hatma yake ni kuibua tabia zisizofaa, kutojipenda, kujiua na kupoteza hali ya uwoga pasi kuzingatia dini, tamaduini na malezi.
Dkt. Kweka ameendelea kufafanua mambo matano ambayo mfanyakazi anatakiwa kuyazingatia ili kuweza kuishi na mtu yeyote na kusema kuwa mambo hayo yana msaada mkubwa kwao na wateja wao kwani watatambua namna ya kusoma hisia za kila mmoja na kubadili njia ya kuweza kusikilizwa au kumsikiliza mtu mwenye changamoto ya afya ya akili na kuyataja mambo hayo ikiwa ni pamoja na kuzuia,kupokea,kubadili muelekeo, na kukubali.
Ameongeza kuwa kati ya mambo hayo matano, matatu hayapatikani darasani bali katika jamii tathmini zinaonesha wafanyakazi wa leo wanakosa vitu vingi katika jamii kwakuwa wamejiwekea mkakati wa maisha yao kwamba wanatakiwa wakitoka kazini kuelekea kanisani ama msikitini kurejea nyumbani bila kujali jamii inayowazunguka ambayo haihitaji gharama kubwa kuweza kuifikia zaidi ya ukarimu na kushirikiana nayo katika mambo ya kijamii tabia inayopelekea wafanyakazi kukosa msaada wa haraka wanapokuwa hawapo nyumbani.
0 Comments