Na: Tatyana Celestine
Ili kuhakikisha wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wanapata uelewa kuhusu Afya ya Akili kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo nchini Menejimenti ya Chuo imeamua kuwapa mafunzo ili kukabiliana na hali hiyo katika utendaji wa kazi wa kila siku pamoja na maisha kwa ujumla.
Muwezeshaji
katika mafunzo hayo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Garvin Kweka
kutoka Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jinini Dar es salaam amesema kuwa
wafanyakazi wanahitaji elimu hiyo ili kujitambua na kufanya kazi kulingana na
mazingira na kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo afya,
hisia, jamii na malezi ya watoto.
Ameongeza
kuwa matatizo ya afya ya akili yamekuwa kwa kasi kutokana na ukuaji wa sayansi
na teknolojia na kufanya mambo mengi kubadilika na kupelekea binadamu kushindwa
kuhimili changamoto zinazowakabili na matokeo yake wanafanya maamuzi ya kujiua, kujiingiza katika mambo yasiyofaa kama
uvutaji shisha, unywaji pombe uliopitiliza, ulaji mbaya vitu ambavyo kupelekea
kupata magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Kisukari na Msongo wa Mawazo hatimaye
kifo.
Dkt. Kweka
amewataka wafanyakazi kuwa wawazi kwa watu wanaowaamini kwani sayansi inasema ili kutibu matibabu
ya afya ya akili asilimia 80 ni kuongea hivyo njia hiyo itawasaidia kutatua
changamoto zao pamoja na kuacha tabia ya kujitenga na jamii kwani kupitia jamii
ufumbuzi wa changamoto hupatikana kabla
na baada ya kustaafu.
Mafunzo
hayo yatatolewa katika Kampasi zote za SUA ambapo yameanza na Kampasi Kuu ya Edward
Moringe Sokoine, Solomoni Mahlangu na baadae kuelekea Kampasi ya Mizengo Pinda iliyoko
mkoani Katavi.
0 Comments