Na: Tatyana Celestine
Katika kuhakikisha ushirikiano na
mawasiliano mazuri kati ya wanafunzi wa ndani na nje ya nchi wa Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo (SUA) kimeamua kupunguza gharama za Ada kwa wanafunzi wa kimataifa
na kufanya SUA kuwa Chuo pekee kinachotoa elimu yenye ubora kwa gharama nafuu
Afrika kwa lengo la kuendelea kuvutia watu wote duniani kujiunga na Chuo hicho.
Akizungumza na wanafunzi kutoka
mataifa mbalimbali katika Siku ya Kimataifa ya SUA kwa niaba ya Makamu Mkuu wa
Chuo Prof. Raphael Chibunda, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Maulid Mwatawala
amesema wanafunzi wote katika Jumuiya ya Africa Mashariki wamepata punguzo la
Ada kwani wameamua kutoa elimu bila
kujali utaifa na kuendelea kufanya Chuo hicho kuwa na hadhi ya kimataifa kwa
kuweka miundombinu rafiki kwa wote wanaopata nafasi ya kusoma hapo.
Prof. Mwatawala amesema Chuo kinaendelea kuimarisha ubora wa elimu kwa kupitia mitaala na kufanya elimu
inayotolewa chuoni hapo kuwa kwa vitendo zaidi pamoja na kuhakikisha mahitaji muhimu ya
wanafunzi wote yanapatikana kikamilifu ili waweze kuishi vizuri wawapo chuoni kwani
nchi ya Tanzania ina makabila zaidi ya 24 hivyo amewataka wanafunzi hao kutumia
fursa hiyo kwa kujifunza Kiswahili wasichukulie hiyo kama ni changamoto kwao
bali fursa na hiyo ndio maana halisi ya kimataifa.
Kwa upande wake Mratibu wa Umataifishaji
na Majalisi SUA Dkt. Jonathan Mbwambo amesema kuwa siku hiyo ya kimataifa SUA
wao wanaitumia kwa kuwaweka pamoja na pia kusikiliza changamoto za wanafunzi wa
kimataifa ili kuendelea kuboresha maisha ya wanafunzi kitaaluma na kawaida
ambapo wataonesha mila na desturi kutoka mataifa mbalimbali ambapo SUA inatumia fursa hiyo kujitangaza kimataifa.
Naye Mwanafunzi wa kimaifa kutoka Zimbabwe Nqobizitha Mpofu amesema hajawahi kujuta kujiunga na SUA kwani elimu na mazingira rafiki ya chuo hicho kwa upande wake SUA ni namba moja Afrika katika kutoa mafunzo ya kilimo kwa ubora kwani tangu amewasili hapo amejionea wakufunzi wakifundisha vema na hakuna changamoto yoyote waliyokutana nayo.
Vilevile Mwanafunzi wa mwaka wa nne
Kozi ya Tiba ya Wanyama Bi. Jtumbisa Tjijembo kutoka Namibia amesema Menejimenti
ya SUA inajitahidi kuwafanya waishi vizuri wakiwa chuoni hapo na hata kuwaandalia
siku kama hiyo inayowakutanisha kwa maana inaashiria Afrika ni wamoja yeye
binafsi kupitia chuo hicho kimemjenga kuona hakuna jambo linaloweza kuwa gumu
kutokana na kuchanganyika watu kutoka mataifa tofauti na kuishi vizuri.
Kupitia siku hiyo mataifa
mbalimbali yameweza kuonesha tamaduni zao kwa mavazi, kuelezea historia ya
mataifa yao, chakula, pamoja na kufurahia nyimbo za kitamaduni ambapo
wanafunzi 105 wakiwemo kutoka Nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,
Lesotho, Comoro, Zimbabwe, Mauritius, Afrika ya Kusini, Botswana.
Nchi nyingine ni Kongo, Liberia, Ethiopia, Eswatini, Namibia, Congo, Berlin, Nigeria na Mozambique yameweza kuonesha namna wanavyoweza kucheza na kupika vyakula vya utamaduni wa mataifa yao.
0 Comments