Na: Gerald Lwomile
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Wiki ya
Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2024 itajenga uelewa na kufungua fursa
nyingi kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Elimu nchini.
Prof. Carolyne Nombo akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Popatlal Tanga (Picha zote na Gerald Lwomile) |
Prof. Nombo amesema hayo leo Mei
26, 2024 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga, na kuwa watu
watapata taarifa za vyuo mbalimbali wanavyoweza kujiunga na wabunifu wa
teknolojia watauza kwa kuzitangaza bidhaa zao.
Prof. Nombo amesema kumekuwa na
teknolojia nyingi zilizozalishwa na vijana ambao wanasoma katika vyuo
mbalimbali nchini, ambazo zimekosa jukwaa la kuzionyesha na namna zinavyoweza
kutatua changamoto mbalimbali hivyo kupitia wiki hii ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu
watapata fursa ya kuzionyesha.
Afisa Udahili kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Bw. Ally Ramadhan (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kufanya udahili mtandaoni. |
Aidha Prof. Nombo amesema kuna
wabunifu wengi nchini ambao wanapata malezi kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia
Tanzania watakutanishwa na wadau mbalimbali ili kubyasharisha teknolojia na ubunifu wao ili uweza kuingiza kipato kwa mtafiti au mbunifu na taifa kwa
ujumla.
Naye Ramadhan Shedoe na Leah
Kavishe ambao ni wakazi wa jijini Tanga wameimbia SUA Media kuwa maonesho hayo
mbali na kuwaletea ujuzi na ubunifu kutoka maeneo mbalimbali lakini pia
yananyanyua uchumi wa Jiji la Tanga.
Bi Leah amesema imekuwa faraja kubwa
kwa wakazi wa Tanga kupata fursa ya kujua ni wapi wanaweza kupeleka watoto wao
kwa mafunzo ya elimu ya juu na elimu ya kati.
Picha chini ni matukio mbalimbali katika banda la SUA
0 Comments