Na: Gerald Lwomile
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) kimesema kinaendelea kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo matumizi ya Akili
Mnemba ili kurahisisha mawasiliano na upatikanaji teknolojia za kilimo na
taarifa sahihi zinazoweza kuwasaidia wakulima katika kutatua changamoto zao.
Joseph Ruboha Mhadhiri Msaidizi na mbobezi katika fani ya wadudu kuitoka Kampasi ya Katavi ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo akitoa maelezo juu ya Nyuki (Picha zote na Gerald Lwomile) |
Hayo yamesemwa Mei 25, 2024 na Mkuu
wa Kitengo cha Ugani kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE – SUA Dkt.
Emmanuel Malisa katika maonesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyoanza
jijini Tanga.
Dkt. Malisa amesema matumizi ya Akili
Mnemna na mawasiliano rahisi yakiwa ni pamoja na kutumia simu za aina zote za
mkononi baina ya mkulima na wataalamu kwa kutumia teknolojia hiyo ya
mawasiliano itatatua changamoto nyingi.
Dkt. Emmanuel Malisa aliyekaa (kulia) na Afisa Msimamizi Mkuu wa Uhaulishaji wa Teknolojia SUA Lucy Madala wakiendelea na maandalizi ya maonesho, |
Sasa tunataka kufikia hatua ya
kutumia Akili Mnemba kuhakikisha kuwa mkulima yeyote ambaye ana simu yake
mahali popote anaweza kupata teknolojia au taarifa iliyotokea SUA kwa wakati,
tayari tumeanza tafiti kidogo kidogo na tunaamini watafiti wetu watakamilisha
hilo” amesema Dkt. Malisa
Maadhimisho ya Wiki ya Elimu,
Sayansi na Ubunifu yameanza leo Mei 25 na yatafunguliwa rasmi Mei 27, 2024, kauli
mbiu ya maonesho hayo ni ‘Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi Shindani’.
Picha chini ni watumishi na wanafunzi kutoka SUA wakiendelea na maandalizi ya maonesho
0 Comments