SUAMEDIA

Wazalishaji Mbegu za Muhogo washauriwa kuzingatia kanuni


Na Idara ya Uhaulishaji wa Teknolojia, TARI

Wakulima wa uzalishaji wa mbegu bora za muhogo wameshauriwa kuzingatia kanuni za uzalishaji wa mbegu ili tija inayokusudiwa katika kilimo cha zao la muhogo kupitia matumizi ya mbegu bora iweze kupatikana.

                                    

Wito huo umetolewa Mei 29,2024 na Dkt. Habai Masunga mratibu wa mradi wa Muhogo Bora katika siku ya mkulima wa muhogo iliyofanyika Kijiji cha Sanjaranda, halmashauri ya  Itigi, Mkoani Singida.

Dkt. Habai, ambaye ni mtafiti kituo cha utafiti cha TARI Ukiriguru amesema tayari wamewajengea uwezo wazalishaji 242 wa mbegu za Muhugo katika maeneo yanayotekelezwa mradi, tisa (9) katika hao wanapatikana katika vijijini na kata mbalimbali zilizopo halmashauri ya Itigi na Manyoni hivyo ni wajibu wao kufuata kanuni hizo.

Amesema miongoni mwa kanuni zinazopaswa kuzingatiwa ni pamoja na kuhakikisha mashamba yao yanakaguliwa na kusajiliwa na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kwa mujibu wa Sheria.

Mbegu bora za muhogo zilizotafitiwa kama (TARICASS1, TARICASS2, TARICASS3, TARICASS4, TARICASS5, KIROBA MKUMBA na KIZIMBANI) zina sifa ya kustahilimili magonjwa ya batobato na michirizi Kahawia.

Pia hukomaa mapema na zinatoa mavuno mengi kati ya tani 25 hadi 50 kwa hekta moja










Post a Comment

0 Comments