Na: Calvin E, Gwabara
Wauguzi katika Hospitali za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) wametakiwa kuzingatia viapo vyao kwa kutoa huduma bora kulingana na
maadili ya kazi kwakuwa umuhimu wa kazi hiyo ndio unaowatofautisha na kazi
zingine ambazo hazitoi viapo kwa taaluma zao.
Kauli hiyo imetolewa na Daktari Mkazi wa Hospitali za SUA Omary Kasuwi wakati akihitimisha Wiki ya Wauguzi ambapo wauguzi kutoka SUA wameungana na wauguzi kote duniani sambamba na hilo wamejikita katika kufanya vipimo na ushauri, usafi katika jamii na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa hospitalini hapo.
“Ndugu zangu nyinyi lazima mtambue kuwa sio kila taaluma
wanapewa viapo vya kazi, kiapo ni kitu kikubwa sana kwa mtu au taaluma ndio
maana unaweza kuona ni taaluma chache sana zinazotoa viapo, Kiapo kina maana
kubwa sana kiroho na kimaadili katika utoaji wa huduma hivyo pamoja na
changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo lakini niwakumbushe kuviishi viapo
vyenu ” amesema Dkt.
Kasuwi.
Daktari Mkazi huyo amesema kuna jitihada kubwa zinafanywa kupitia hospitali na Menejimenti ya SUA katika kupunguza baadhi ya changamoto walizoainisha hivyo
amewataka kuendelea kufanya kazi kwa moyo kuhudumia jamii na pindi fedha
zitakapopatikana changamoto hizo ikiwemo uchache wao na mahitaji mengine
yatatatuliwa ili kuzidi kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
Kwa upande wake Matroni wa Hospitali za SUA Bi. Akaanashe
Makere amepongeza Menajimenti ya SUA kupitia kwa Dkt. Kasuwi kwa namana
anavyopigania Kurugenzi ya Afya chuoni hapo na fani ya uuguzi kwa pamoja kwa
kuweka kipaumbele zaidi kuona huduma bora zinatolewa kwa wanaohitaji taaluma
yao hasa katika kupigania upatikanaji wa madawa na vifaa tiba huku akihakikisha
utoaji huduma unakuwa rafiki kwa wafanyakazi wote
“Umekuwa ukijitolea muda wako mwingi sana kutupatia elimu sehemu
za kazi ili kuboresha utendaji wetu hivyo tunakuahidi kuwa tutazidi kufanyia
kazi yale yote unayotuelekeza na tutakuwa bora zaidi lakini niwatake pia
wauguzi wenzangu kujiendeleza katika nyanja mbalimbali pale fursa inapopatikana
na tutumie mitandao kujiendeleza na masomo tunayopata mara kwa mara wakati wa
vikao vya kila siku asubuhi kwaajili ya kupata alama za kuhuisha leseni zetu”
Ameeleza Matroni Makere.
Akisoma Risala ya wauguzi kwa niaba ya wauguzi wenzake Bi.
Joraphina Manyelezi amesema siku ya wauguzi duniani huadhimishwa tarehe 12
mwenzi mei kila mwaka kwa lengo la kumuenzi muasisi wa taaluma ya wauguzi
dunaiani aliyefahamika kwa jina la Florence Nightingale aliyefanya kazi kwenye
mazingira magumu vitani akiwahudumia majeruhi usiku na mchana kwa kujitolea na
baadae huduma hii ya uuguzi iliendelea kuboreshwa katika mazingira ya utoaji
huduma na pia uandaaji wa mitaala ya kufundishia.
“ Lengo la maadhimisho haya ni kukumbushana kuhusu taaluma, wajibu wa kazi ya uuguzi na
maadili yake na katika kutekeleza lengo la maadhimisho haya wauguzi wa SUA
tulijumuika kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kupima
shinikizo la damu, Sukari, Maambukizi ya VVU kwa hiari pamoja na elimu ya afya” amesema Bi.
Munyerezi.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania Tawi la SUA Bwana
Priscus Nassoro amewapongeza wauguzi wote kwa kujitoea kwa hali na mali
katika kufanikisha maadhimisho hayo chuoni hapo bila kujali uchache wao na
kushukuru Uongozi wa hospitali kwa ushirikiano kuwezesha wauguzi hao kupewa
ruhusa kuadhimisha siku hiyo muhimu kwao.
“Kwakweli kupitia shughuli za upimaji tulizozifanya kwanza
tushukuru jamii kujitokeza katika kupata vipimo na ushauri lakini tuseme tuu
kuwa jamii yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiafya hivyo tunaahidi
kuendelea kushirikiana na Chuo na Serikali yetu katika kupunguza changamoto
hizo kwa kufanya kazi kwa weledi lakini pia mwakani tunatarajia kufanya vizuri
zaidi kwa kuanza maandalizi mapema” amefafanua Bw. Nassoro.
Katika kuhitimisha shughuli hiyo wametoa zawadi pia kwa
Daktari Mkazi wa Hospitali za SUA ambaye nae amewapa zawadi kwa kazi yao nzuri lakini
pia wamekula kiapo cha uaminifu na utiifu katika kazi sambamba na kauli mbiu
yao ya mwaka huu isemayo “Wauguzi sauti
inayoongoza, wekeza katika uuguzi,heshima haki linda Afya”.
MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE KUHITIMISHA WIKI YABWAUGUZI DUNIANI.
0 Comments