Na :Josephine Mallango
Mkoa wa Morogoro umetajwa kuwa ni mkoa salama kwa utalii ambao una nyongeza ndani yake ya kuwa na njia za utalii na maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii vilivyomo mkoani humo. .jpg)
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya wanahabari zaidi ya 30 ambao pia amewateuwa kuwa wanakamati wa hamasa ya utalii mkoani Morogoro.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMPA) kwa kushirikiana na TANAPA, Malima amewataka wanahabari kuendelea kutangaza vivutio vyote vilivyomo mkoani Morogoro sanjari na wawekezaji kuja kuwekeza hotel za kitalii ndani ya mkoa huo.
"Mkoa wa Morogoro umebarikiwa ni Mkoa wenye vivutio na vile vile watalii wanapita kwenda kwenye utalii katika mikoa mingine na wenyewe Morogoro una hifadhi tatu Udzungwa , Mwalimu nyerere na Mikumi ambayo ina mpaka mnyama Simba kipenzi cha watalii wengi, bado kuna vivutio ikiwemo chemchem ya maji moto Kisaki, vinyonga wa kipekee katika hifadhi asili ya Uluguru ila tujuwe wazi uwepo wa utalii pekee hautoshi tuanze na hamasa kutoka kwa wanahabari na wawekezaji wajitokeze kujenga hotel katika maeneo hayo ya utalii ikiwemo Mikumi, Ruaha , Kilombelo na Morogoro", amesema Malima.
Kwa upande wake Afisa Maliasili na Utalii mkoa wa Morogoro Joseph Chuwa amesema mkoa huo uko katikati na una vivutio vingi vya utalii vya kipekee ambavyo bado havijatumika ipasavyo katika kufungua utalii ambao utaongeza ajira na mapato kwa mkoa na Taifa.
"Bado mkoa haujatumia vivutio vilivyopo katika kujikwamu , kuna vivutio ikiwemo Mazimbu makazi ya zamani ya waafrika Kusini waliopigania Uhuru, kuna makaburi kule, waafrika Kusini wanahitaji kila mwaka pawe vile vile, Mandera aliishi pale kwenye harakati akiwa bondia , utalii huo upo Morogoro pekee, waandishi tangazeni vema utalii katika kuleta fursa mpya ndani ya mkoa wetu", amesema Chuwa.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMPA) Simon Mkina amesema wamekutana na waandishi wa habari Morogoro kuwapa mafunzo juu ya kuandika habari za vivutio vya utalii Morogoro ambavyo vipo na havijulikani kwa kuwa utalii ni moja ya kichocheo za uchumi.
Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke Amiri Abdi amesema utalii ni moja ya sekta inayotoa ajira kwa vijana na kwamba takwimu kutoka kwa Mtakwimu Mkuu na Benki ya Tanzania zinaonesha kuongezeka kwa watalii nchini kutoka milioni 1.5 mwaka 2022 mpaka milioni 1.8 mwaka 2023.
Mkufunzi huyo ameongeza kuwa mpango wa Serikali wa sasa chini ya Rais Samia Suhuhu Hassan ni kufikia wataliii milioni 5 ifikapo 2025 , hivyo juhudi za mkoa wa Morogoro zinazoendelea ikiwemo Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima kukubali kufufua utalii na kutangaza vivutio vilivyopo zinashabihiana na kasi ya taifa ya mwaka 2025.


0 Comments