Na: Siwema
Malibiche,
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)
wameaswa kutumia elimu na mafunzo waliyopata
chuoni hapo kwa ubunifu
katika kufanya ubunifu wa
maendeleo endelevu kwa ustawi wa taifa
la Tanzania.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed
Chande Othman wakati wa hotuba yake ya utekelezaji wa majukumu ya Chuo kwenye
mahafali ya 43 ya katikati ya mwaka ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye Kampasi
ya Edward Moringe mkoani Morogoro ambapo jumla ya wanachuo 777 wamehitimu 777 masomo
yao.
Amesema
Baraza la Chuo limeendelea kutekeleza majukumu kwa ufanisi, majukumu hayo ni pamoja na kuisimamia
Menejimenti ya Chuo ili itekeleze majukumu makuu ya Chuo ambayo ni pamoja na kutoa
mafunzo, kufanya utafiti, kutoa huduma za Kitaalamu, pamoja na shughuli za
ugani.
Aidha amesema SUA
inawatarajia wahitimu hao wawe
mabalozi wa kukitangaza Chuo vizuri kwa tabia na utendaji wao mzuri wa kazi
lakini pia ni mategemeo ya Chuo kwamba watatumia elimu waliyopata kwa kufanya
kazi kwa bidii, weledi na ubunifu kwa
maendeleo ya nchi.
"Mnapoingia
kwenye ulimwengu wa ajira iwe ya kuajiriwa au ya kujiajiri kumbukeni
kuwa nyinyi ni mabalozi wetu katika kutunza maadili , ubunifu, na uchapakazi,
maarifa na ujuzi mlioupata hapa ziwe dhana za kuleta mabadiliko
chanya kushughulika na matatizo
ya nchi na za kidunia na kuboresha maisha
ya watanzania na jamii kwa
ujumla," ameeleza Jaji uyo
Mstaafu.
Vile vile
Jaji huyo amewataka wahitimu kuyaishi maneno ya hayati Nelson Mandela ambayo
yanasema elimu ndiyo silaha yenye nguvu zaidi
ambayo inaweza kutumia nguvu
nyingi zaidi katika kubadilisha ulimwengu na anaamini
kuwa wahitimu hao wana uwezo wa kuubadilisha ulimwengu.
Kwa upande wake Goodluck Saltiel Maoy muhitimu wa Shahada ya Uhifadhi wa Wanyama Pori
SUA ameipongeza Menejimenti ya Chuo kwa kuandaa sherehe za mahafali huku akiwataka wahitimu
wenzake kuyaishi kwa vitendo yale yote
ambayo wamejifunza katika kipindi chote
cha masomo chuoni hapo huku akikisisitiza kuwa yeye ataenda kuongeza elimu kwa
jamii kuhusu namna nzuri ya kuhifadhi wanyamapori ili kukuza utalii nchini.
Naye
Nicodemo Charles Mahega muhitimu wa
Shahada ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia
amesema anaenda kuisaidia jamii huku akiweka wazi kuwa anatambua uwepo wa
changamoto hasa kwenye mfumo wa chakula
Tanzania na kutokana na elimu aliyoipata
italeta chachu kwenda
kuibadilisha jamii juu ya matumizi
mazuri ya lishe na kutoa wito kwa jamii
kushirikiana na wataalam wa
lishe ili kuhakikisha uwepo wa
lishe bora kwa watanzania wote.
0 Comments