Na: Calvin Gwabara – Morogoro.
Jumuiya ya Watafiti nchini wametakiwa kufurahia maisha ya Marehemu Dkt. Leonard Ernest Gustavin Mboera badala ya kusikitika kwakuwa kazi kubwa alizozifanya wakati wa uhai wake zinaendelea kuishi na kutoa mchango mkubwa kwa jamii na Taifa.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kigoda cha Utafiti cha
Oliver Tambo cha Magonjwa ya Virusi na Kiongozi wa kituo cha Umahiri cha
magonjwa ya kuambukiza na afya Moja cha SACIDS kilichopo Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo Prof. Gerald Misinzo wakati
akitoa salamu za Kituo hicho na SUA kwenye kipindi maalumu cha kumpa heshima na
kutambua mchago wa marehemu Dkt. Mboera kwenye mkutano wa kisayansi wa 40 wa
chama cha afya ya jamii Tanzania TPHA na mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho
unaofanyika mkoani Morogoro.
“Kwa watu wote tunaomfahamu na tuliopata nafasi ya kufanya
kazi na Mpendwa wetu Marehemu Dkt. Leonard Ernest Gustavin Mboera hatuna sababu
ya kuendelea kuhuzunika, tunachopaswa kufanya ni kusherehekea maisha yake
kwakuwa ni mtu ambaye aliyatumia maisha yake yote kusaidia kutafuta suluhu ya
matatioz mbali ya Jamii yetu na ameandika machapisho mengi kwenye majarida
yenye heshima kubwa duniani ambayo mpaka sasa yanaendela kutumiwa na
wanasayansi mbalimbali kote ulimwenguni” alisema Prof. Misinzo.
“ Sote tunatambua na hasa mimi kuwa nimefanya kazi nae katika
kuandika miradi mingi ya utafiti yenye maana kubwa kwa taifa ambayo tuliipata
na imesaidia sana katika kutatua changamoto mbalimbali za afya ya jamii zetu
lakini pia fedha hizo zimesomesha wanafunzi wengi kutoka ndani nan je ya
Tanzania, na kwakuwa alikuwa mtu anayependa kusimamia maandiko yenye viwango
alisimamia Wanafunzi wengi n ahata hapa kwenye mkutano huu wapo kuwasilisha
matokeo yao hii ni kazi yake kubwa aliyoipenda na kuisimamia kwa moyo wake wote
ukiacha kuwa mhariri wa majapisho yenu”.
Awali kifungua Mkutano huo Mkuu wa Kisayansi wa TPHA
aliyekuwa naibu waziri wa afya ambaye sasa ni Mbunge wa Kigamboni na Makamu mwenyekiti
wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii Mhe. Dkt. Faustine Ngugulile amesema TPHA
imesheheheni wanachama nguli, Waandamizi na waliobobea kwenye masua ya afya
Tanzania hivyo ni wakati sasa wakajitokeza na kutoa mchango wao kwa taifa na
kuwa mshauri mkuu wa Serikali kwenye masula mbalimbali yanyohusu afya nchini.
“Ukiangalia watu mlionao mambao ndio wanachama wenu ni watu
wenye heshima kubwa sana kwa taifa kwenye sekta ya afya natamani kuona kuwa
TPHA inakuwa chombo cha ushauri kwa Serikali katika masuala yote ya afya na
hili litawezekana kama viongozi mtatoka na kuonesha kazi ambazo chama chetu
hiki kinafanya na kuifanya serikali ijue ili iwee kuwatumia vilivyo” alifafanua
Mhe. Dkt. Ndugulile.
Mhe. Dkt. Ngudulile ameitaka TPHA kuwa inaandaa makongamano
makubwa ambayo yatahusisha watunga Sera, Viongozi wa Serikali na wadau wengine
kwakuwa wao ndio watumiaji wa kazi wanazozifanya kama chama huku akitambua
mchango mkubwa wa serikali kuboresha sekta ya afya kwa kupambana na magonjwa
mbalimbali ambayo yalikuwa yakipoteza nguvu kazi ya taifa lakini pia kusaidia
sasa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma kuanzia kijiji hadi Taifa na
kupunguza idadi ya wagonjwa kupelekwa nje ya nchi kwa asilimia 90 kupata huduma
hizo hapa nchini katika ubora uleule.
Akieleza malengo ya mkutano huo Mkuu wa 40 wa Kisayansi wa
Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) Mwenyekiti wa chama hicho Dkt. Mariam
Ongara amesema pamoja na mda kuu ya mkutano huu lakini kuna mada zingine
ndogondogo saba ambazo pia ni kati ya vipaumbele 10 vya Wizara ya Afya
vilivyowasilishwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa Bunge la bajeti
linaloaendelea Jijini Dodoma katika bajeti yake.
“Tunatarajia kuvijadili na kuvitolea mapendekezo na mwisho
tunwasilisha mapendekezo hayo Serikalini na tunashukuru sana Serikali imekuwa
ikifanyia kazi mapendekezo yetu ambayo tumekuwa tukiyawasilisha kwenye kila
mkutano wetu mkuu hali ambayo inatufanya tuendelee kutoa mapendekezo chanya kwa
manufaa ya afya ya watu wetu na Taifa kwa ujumla” alisema Dkt. Ongara.
Wanchama wa chama cha afya ya jamii wametumia nafasi hiyo
kumpongeza Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuteuliwa na Serikali kugombea
nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la afya Duniani Kanda ya Afrika na kumtakia
mafaniko mema kwenye nafasi hiyo kubwa kimataifa ambayo anapigiwa kura na
mawaziri wa afya wa nchi 47 za Afrika.
Mkutano huo wa 40 wa mwaka wa Kisayansi umebeba Kauli mbiu
isemayo “Kuboresha hafua za afya ya jamii na utoaji huduma: Furasa na
Changamoto.
Mwenyekiti wa TPHA Dkt. Mariam Ongara akieleza malengo ya mkutano huo Mkuu wa 40 wa Kisayansi wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA).
0 Comments