SUAMEDIA

Teknolojia ya malisho ya SUA inaweza kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji

 Na: Gerald Lwomile

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga Ustadhi Rajabu Abdallah, amesema teknolojia ya malisho iliyofanyiwa utafiti Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ni suluhisho la migogoro ya wakulima na wafugaji.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga Ustadhi Rajabu Abdallah (aliyevaa kofia nyeupe) akisikiliza maelezo juu ya Hospitali ya wanyama inayotembe. 

Ustadhi Rajabu Abdallah amesema hayo leo Mei 29, 2024 alipotembelea Banda la SUA katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu iliyoanza tarehe Mei 25, 2024 jijini Tanga.

Amesema katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo mkoa wa Tanga kumekuwa kukitokea ugomvi na wakati mwingine mapigano kati ya wakulima na wafugaji kutokana na mifugo kula mazao ya wakulima wakati wa malisho.

Ustadhi Abdallah amesema teknolojia ya malisho ambayo mfugaji anaweza kuwa na eneo lake na kupanda malisho ambayo hustawi sana inaweza kuondoa tatizo baina ya wakulima na wafugaji.

Nao waoneshaji kutoka SUA Bw. Mikidadi Rashidi ambaye ni Mtalamu wa Maabara na Joseph Ruboha ambaye ni Mtafiti SUA wameiambia SUA Media kuwa maadhimisho hayo yana tija kubwa kwa wakulima na wafugaji kwani yatawaongezea maarifa na ujuzi.

Mikidadi Rashidi amesema wamekuja na chanjo ya Samaki aina ya Sato dhidi ya ugonjwa wa kuvilia damu unaosababishwa na bacteria aitwaye Aeromonas hydrophila ambayo imeshafanyiwa majaribio katika mikoa ya Ruvuma, Arusha na Mwanza na kuonyesha ufanisi wa zaidi  ya asilimia 90.

Kusikiliza zaidi bofya hapo chini 👇

https://www.instagram.com/reel/C7jJzJrIEHr/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Naye Joseph Ruboha amesema ni muhimu watu wakajua umuhimu wa Nyuki katika Bioanuai kwani huenda kungekuwa na changamoto kubwa katika uzalishaji wa mazao kwani nyuki wanasaidia katika uchavushaji wa mazao.

Aidha amesema mbali na Asali, Nyuki wana uwezo wa kutoa mazao kadhaa ikiwemo Shampoo, Mafuta ya kupaka na kuchua na Mishuma.

Kusikiliza zaidi bofya hapo chini 👇

https://www.instagram.com/reel/C7jgPWxI2Vi/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe (aliyevaa kofia nyeupe) akiwa katika Banda la SUA

Msanii Maarufu nchini Mrisho Mpoto naye amentembelea banda la SUA

Chini ni picha mbalimbali katika banda la SUA 👇






Post a Comment

0 Comments