Na: Gerald Lwomile
Imeelezwa kuwa utashi wa kisiasa,
ukweli kuhusu kuingia kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda na kutatua changamoto
mbalimbali ni baadhi ya mambo ambayo hayakwepi na suluhisho lake ni kuwa na
teknolojia bora na elimu ya amali.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo |
Hayo yamesemwa leo Mei 28, 2024
na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,
wakati akizungumza katika Kongamano la Elimu, Ujuzi na Ubunifu lililofanyika
katika ukumbi wa Tanga Beach Resort jijini Tanga.
Prof. Nombo amesema mafunzo ya amali ambayo miaka ya nyuma yalikuwa yakifundisha tangia shule za msingi na sekondari na yalijulikama kama Sayansi Kimu kwa shule za msingi na katika shule za sekondari wanafunzi walisoma Uhandisi, Mapishi, Kilimo na masomo mengine mengi ambayo yalimuandaa kijana kuwa na ujuzi na kumuweka katika soko la ushindani kwa kupata ajira au kujiajiri.
Amesema tayari vyuo vikuu vina
miongozo kuhusu aina hii ya elimu na vimeeendelea kujenga mahusiano mazuri na
viwanda binafsi ili kuhakikisha mwanafunzi anapata zaidi mafunzo ya vitendo ya
fani anayochukua.
Akizungumza katika kongomano hilo,
Mwenyekiti Mtendaji wa AfricAcademy-Arusha Science na Mhadisi Kilimo Prof. Nuhu
Hatibu amesema mifumo mingi hivi sasa inatumia teknolojia za kisasa hivyo kama
taifa hakuna sababu ya kusubiri na watu hasa vijana na watoto kuonyeshwa njia
ya kuasili mifumo hii.
Akizungumzia mifumo ya kidijiti Bi.
Winfred Ng’ang’a kutoka Kampuni Tanzu ya ‘Amazon Web Services’ ya nchini
Kenya ambayo hutoa huduma za kidijitali kwa kutumia mfumo wa uandaaji wa
program kidijiti wao wamefanikiwa kuhakikisha wanafunzi katika nchi ya Kenya
wanakuwa na jukwaa ambalo linawasaidia kupata taarifa mbalimbali na pia wanaweza
kuwa taarifa zao.
Bi. Winfred Ng’ang’a kutoka Kampuni Tanzu ya ‘Amazon Web Services’ ya nchini Kenya akielezea uzoefu wa Kampuni yao ya AWS |
0 Comments