Na:Tatyana Celestine- Mwanza.
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeendelea kuunga mkono Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alilolitoa katika Mkutano wa 10 mjini Zanzibar la waajiri kuwapa nafasi ya kushiriki mikutano ya kitaifa ya Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) ambapo 2024 katika Mkutano wa 11 unategemewa kufanyika jijini Mwanza na Mgeni Rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.
Katika kutimiza agizo hilo la Rais Samia Menejimenti ya SUA imetoa zaidi ya shilingi Milioni 40 kufanya zaidi ya Makatibu Mahsusi 25 kushiriki mkutano huo na tayari wamekwisha wasili jijini Mwanza kwa kuanza vikao vyao ambapo leo tarehe 20/05/2024 wameanza kufanya usajili na taratibu nyingine zitakazowawezesha kushiriki vikao hivyo vya kitaaluma hatimaye Mkutano Mkuu wa 11 utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25/05/2024.
Aidha kwa siku zote kuanzia tarehe 20-24 shughuli hizo zitafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza zitahusisha mada
mbalimbali katika kuwajenga kitaaluma, kuwakumbusha wajibu wao katika kazi pamoja
na kuzingatia maadili na Uadilifu wawapo kazini ikiwemo Usimamizi wa mikataba
ya Utendaji, Ushughulikiaji wa Mrejesho, Muundo ya Maendeleo ya Utumishi wa
Kada ya Wandishi waendesha ofisi.
Mkutano huo wa 11 umebeba Kauli Mbiu
isemayo “Mafanikio Huanza na Uamuzi Bora wa Utendaji, Tutumie Muda Vizuri kwa Kufanyakazi na Kuleta Tija”.
KATIKA PICHA MAKATIBU MAHSUSI
TANZANIA (TAPSEA)-SUA WAKISHIRIKI KUFANYA USAJILI MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA
VIWANJA VYA CCM KIRUMBA MWANZA.
0 Comments