Na: Siwema Malibiche
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
mkoani Morogoro limewataka wafanyakazi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
ambao wameshiriki mafunzo ya kukabiliana na majanga mbalimbali kuwa mabalozi
wazuri na kuielimisha jamii namna ya kukabiliana
na hali hiyo inapojitokeza.
Wafanyakazi SUA wakishiriki katika zoezi la majaribio ya kuzima moto katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine |
Akizungumza katika mafunzo ya siku mbili yanayofanyika katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine kuazia Mei 20, 2024 Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro Veronica John amesema Jeshi hilo linapofanyakazi ya uoakoaji hakuna gharama yoyote inayotozwa kwani huduma zote zinatolewa bure.
Amesema ni vyema washiriki kuzingatia
kwa makini mambo yote watakayojifunza hasa tahadhari katika makazi na namba bora ya kukabiliana na
majanga yakiwemo ya moto ambayo hugharimu Maisha na mali za watu.
Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro Veronica John akiongea na wafanyakazi wa SUA, hawapo pichani (Picha na zote na Ayoub Mwigune) |
Aidha amewataka wananchi kuachana
na ujenzi holela ambao unasababisha kuchelewa kwa waokoaji kufika katika eneo
lilitokea janga na badala yake jamii ishirikiane na Jeshi hilo katika usomaji
wa ramani ili kuwa na mpangilio mzuri wa majengo utakaowezesha uwepo wa miundombinu
rafiki.
Kwa upande wake Jumanne Yusuph, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Wasaidizi SUA amelipongeza Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa
kutoa mafunzo ya kinga na tahadhari kwa wafanyakazi SUA na ametoa wito kwa wafanyakazi wote waliopata
mafunzo hayo waende kutoa elimu kwenye jamii kuanzia ngazi ya familia na hasa kwa
watoto ili kusaidia kuongeza tahadhari, kupunguza na
kuepusha madhara yanayoweza
kujitokeza.
Nae Lucas Iyera mshiriki
katika mafunzo hayo ameupongeza uongozi wa Chuo kwa kushirikana na Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji kuandaa mafunzo hayo
ambayo yanasaida kuwakumbusha
namna mwananchi anaweza kuchukua
tahadhari katika kujikinga na majanga
mbalimbali.
Picha chini ni watu ni matukio mbalimbali katika mafunzo hayo
0 Comments