Na: Tatyana Celestine, Mwanza.
Waandishi Waendesha Ofisi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametoa
shukrani zao kwa Menejimenti ya SUA kwa kuona umuhimu wa kuwapa nafasi ya
kujifunza na kukumbushwa maadili ya kazi yao kwani wanayo nafasi ya kujenga au kubomoa
taswira ya Taasisi kutokana na Tabia au Utendaji kazi wawapo ofisini.
Wakizungumza na SUA MEDIA wakati wa Mkutano wa 11 TAPSEA jijini Mwanza
leo Tarehe 21/05/2024 wamesema kuwa Chuo kimekuwa kikiwajali na kuwapa
kipaumbele katika kila nyanja na zaidi katika kuboresha utendaji kazi wao kwa
kujifunza mambo mapya pamoja na kukutana na wengine kila mwaka kwenye Mkutano
wa TAPSEA.
Akielezea namna mafunzo hayo yanavyoweza kuboresha taswira ya Chuo Bi.
Ritha Mashambo ambaye ni Katibu Mahsusi kutoka Kurugenzi ya Mipango na
Uwekezaji- SUA amesema kuwa katika mkutano huo wanajifunza mambo mengi lakini
kubwa zaidi ni utunzaji wa siri za ofisi kwa nafasi hiyo wao ndio hushika
nyaraka mbalimbali kila siku hivyo pasi kukumbushwa umuhimu huo mara kwa mara
ni rahisi kuweza kwenda kinyume na maadili ya kazi.
Mwandishi Muendesha Ofisi huyo ameongeza kuwa wao ni kioo cha ofisi ama
Taasisi kwakuwa wanatengeneza picha halisi kwa namna wanavyotoa huduma kwa
kuonekana Taasisi ni nzuri au mbaya mara nyingi chanzo kinaanzia kwao, hivyo
wanapongeza menejiment kwa kutoa nafasi
na kuona umuhimu wake lakini pia amenashauri
menejimenti kuendelea kutenga fedha kwa
kufanya wote waweze kushiriki kila mwaka.
Kwa upande wake Bi. Romana Kibua ambaye ni Mwandishi Muendesha Ofisi
kutoka Ndaki ya Kilimo SUA amesema mafunzo hayo ni muhimu kwakuzingatia kuna waandishi
waendesha ofisi wapya wanakuwepo kila mwaka hivyo ameomba Mradi wa HEET usiache
kuwashika mkono katika matukio muhimu kama hayo ambayo yanajitokeza mara moja
kwa mwaka ili kuendelea kuwa bora katika kazi.
Katika kuhakikisha mafunzo hayo yanaenda kama ilivyotakiwa menejimenti ya
chuo imeteua muongozaji wa msafara huo nae alipotakiwa kuzungumzia hali halisi
na sababu za yeye kuwepo tofauti na
miaka mingine Afisa Tawala Bi. Eliza Mtambo amaesema kuwa Menejiment imetambua
umuhimu wa mkutano huo na kumtuma yeye ahakikishe kila mmoja aweze kushiriki
kikamilifu katika mafunzo hayo kwani hata wawapo Mwanza haimaanishi hawapo
kazini lazima wazingatie uadilifu, heshima, uchapakazi na maadili ya utumishi.
Aidha Bi. Mtambo amewataka viongozi wanaoandaa Mkutano wa TAPSEA kuanza kufanya maadhalizi mapema hasa katika usajili ambapo kwa mwaka huu wanatumia teknolojia mpya ya usajili (Control Number) ili kuondoa sintofahamu kwa wale ambao wamelipia na wamefika hawaruhusiwi kuinguia moja kwa moja badala yake wanakaa nje kwa muda mrefu kutokana hilo inapelekea washiriki kushindwa kupata kile walichotarajia kwa kukosa kujifunza mada muhimu.
0 Comments