Na: Tatyana Celestine
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepongezwa kuzingatia kutoa
fursa kwa Waandishi Waendesha Ofisi wageni waliohamia, waliobadilisha Kada na
kwa mara ya kwanza kutoka Kampasi ya Olmotonyi wameweza kushiriki katika
kujifunza mafunzo mbalimbali ambayo yatawasaidia katika majukumu yao ya kila siku
kazini hata kwenye familia zao.
Akizungumza na SUAMEDIA Mwenyekiti wa Waandishi Waendesha Ofisi SUA Bi. Joyce
Mwiyola amesema kwa miaka miwili sasa kumekuwa na mabadiliko ya madhurio katika
Mkutano huo kwa upande wa SUA kwani wamekuwa hawashiriki wote hivyo ameomba
menejimenti ya SUA kujitahidi kuhakikisha wanashiriki wote kwani mafunzo hayo
hayajirudii na ni ya muhimu kwao.
Kwa upande wake Mwandishi Mwendesha Ofisi kutoka Kampasi ya Olmotonyi SUA-
Arusha Bi. Abia John amesema anaishukuru
Menejimenti ya SUA kwa kuwakumbuka mwaka huu kushiriki kwa mara ya kwanza
binafsi amejifunza mengi aliyokuwa hayajui ambayo yanamfanya aende kutenda kazi
zake kwa weledi na ubora.
Aidha ameomba kutoishia hapo wazidi kuwafikiria hata wale ambao wapo
katika kampasi nyingine kushiriki kwa miaka ijayo kutokana wanapokosa mafunzo
hayo hawatapata tena na hii ni kutokana na TAPSEA kuhakikisha wanagusa kila
eneo ikiwemo Afya ya akili, Maadili katika kazi, utunzaji wa siri za ofisi kubadilika
kila mwaka.
Kwa kujibu changamoto iliyowasilishwa na muongoza msafara kutoka SUA Afisa
Tawala Bi. Elizabeth Mtambo ya kuwataka viongozi wanaoandaa Mkutano wa TAPSEA kuanza
kufanya maadhalizi mapema, SUA MEDIA imetaka ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa
Waandishi Waendesha Ofisi TAPSEA Morogoro Bi Hellen Magati amesema changamoto
imekuwepo kutokana na upya Teknolojia ya kufanya usajili hivyo amewataka
wanachama wote kuhakikisha wanajisajili kupitia online ili kuondokana na
adha kama iliyojitokeza kipindi hiki.
0 Comments