Na: Tatyana Celestine
Waandishi Waendesha Ofisi wametakiwa kutambua asilimia 80 katika utendaji
wao ni kuhakikisha wanaweka mambo yaende sawa katika ofisi lakini wasiache
kuzingatia afya wawapo mahala pa kazi kwani sayansi inasema kukaa muda mrefu ni hatari zaidi kuliko ulaji mbaya ambao upelekea vifo vingi.
Katika Mkutano wa 11 TAPSEA jijini Mwanza Mwezeshaji ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo Garvin Kweka kutoka Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jinini Dar es salaam akizungumzia Afya ya akili amesema kuwa Waandishi Waendesha Ofisi wanatakiwa watambue maisha yanahitaji Afya ya mwili, Hisia, dini kwa kuwa vitu vyote hivi vitapelekea mwanadamu kuwa na maisha marefu na kuwaepushia magonjwa yasiyo ya lazima lakini pia kuyakabili.
Daktari huyo ameweka bayana kwamba matendo ya mwanadamu anayoyafanya katika umri alionao ndio yanapelea kuishi kwa afya bora au la hapo baadae kwani wagonjwa wengi magojwa yao huchangiwa na tabia hatarishi kama vile ulevi, ulaji mbaya na zinaa ambazo ndio zinakusanya magonjwa yote yanayotesa watu kwa sasa.
Aidha amesema wafanyakazi wengi wanaangalia zaidi namna ya upatikanaji wa
pesa na mali na kusahau afya zao bila kujua mwanadamu anapofika umri kuanzia
miaka 40 ndio anatakiwa kuzingatia afya zaidi kuliko utafutaji wa mali na fedha
maana hata akizipata hawawezi kuzitumia vizuri ikiwa afya yake sio nzuri
matokeo yake gharama kubwa za matibabu hutumika kwa kutibu maradhi ambayo
yangeweza kuzuilika hapo kabla.
Pia Dkt. Kweka ameeleza kuwa Waandishi
Waendesha Ofisi wasipozingatia Afya wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya
mifupa, mgongo, mumivu ya mwili, unene ulipitiliza, saratani, kisukari ambayo
yatakulazimisha utumie dawa matokeo yake wanaweza kuua figo hivyo kuanzia sasa
waangalie viti wanavyotumia kukaa ofisini, unywaji wa maji, kula kwa kiasi
pamoja na mazoezi.
Katika upande mwingine amewaasa wafanyakazi ambao wanashindwa kuzingatia
malezi ya watoto wao kwa kuwapa kila kitu wanachotaka kula pasi kuzingatia
chakula bora matokeo yake wanaanza kuugua magonjwa kama kisukari na moyo wakiwa
wadogo huku wazazi wengine kushindwa kuwalinda watoto wao kupelekea majanga
kama ubakaji, ulawiti, uvutaji shisha, ulevi hatimaye wakija kugundua tatizo
linakuwa limekwishakuwa kubwa hivyo wafanyakazi wasiwasahau watoto hata kama
wana kazi nyingi.
0 Comments