Na: Siwema Malibiche
Wizara
ya Kilimo na Uvuvi kwa kushirikina na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) wameendesha mafunzo kwa wataalamu
wa Tiba za wanyama Tanzania Bara na visiwani
katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) yenye malengo ya kukuza uelewa katika
sayansi ya wanyama Tanzania.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Charles Mhina akifungua mafunzo (Picha zote na Ayoub Mwigune) |
Dkt Mhina
amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi
inatambua umuhimu mkubwa wa kilimo na mifugo nchini katika kukuza ubora wa afya
za jamii kwa kuboresha mazingira mazuri
kwa wanyama huku lengo kuu likiwa ni kupata
tija kupitia mifugo hiyo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla na serikali itahakikisha kuwa mafunzo haya yatakuwa
endelevu ili kuendelea kukuza uelewa kwa
wataalamu wote nchini.
Pia
ametoa shukrani kwa SUA na FAO kwa
kutoa ushirikiano wao thabiti na serikali
kwa kuendelea kutoa mafunzo endelevu
kwa wataalamu wa afya ya wanyama na binadamu nchini kwa kushirikiana na serikali kwa lengo la
kuisadia jamii kuondokana na
changamoto katika sekta ya uvuvi na
mifungo ikiwemo magonjwa ya mlipuko
kwa kuyatafutia ufumbuzi wa haraka.
Naye,
Prof Ezra Karimribo Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi ya Afya kutoka
SUA ameupongeza uongozi wa chuo kwa kuendelea kuwa wadau wakubwa katika utoaji
wa mafunzo kwa wataalamu wa mifugo na
kuongeza kuwa katika mafunzo haya SUA imeusika katika kuandaa mtaala ma
mafunzo hayo. Na amewataka washiriki
wote kuyafanyia kazi yale yote
watakayojifunza katika kipindi chote cha mafunzo ili kuleta tija kwa taifa.
Prof Ezra Karimribo Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi ya Afya kutoka SUA akifuatilia mafunzo hayo |
Ameongeza
kuwa mafunzo hayo ni mazuri kwa sababu yatasaidia kutambua changamoto
zinazowakabili wanyama kwa haraka na kuanza kuchukua tahadhari.
Kwa upande
wake, Zehra Zam kutoka Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji Maliasili na Mifugo kutoka Zanzibar
amesema mafunzo hayo yatasadia
kukuza ubora wa huduma wanazozitoa kwa jamii na ametoa rai kwa wafugaji wote nchini
kuwa makini katika kuzingatia hali ya usafi
ndani ya kipindi cha mvua kwa mifugo yao
kwa kuhakikisha uwepo wa chakula
bora, matibabu na mazingira mazuri wanayoishi wanyama hao
ili mifugo iweze kuwa na afya bora itakayokidhi ubora wa kimataifa.
Naye
Dkt Ally
Mohamed Mkuu wa Mifugo Zanzibar amesema mafunzo hayo yatasaida
kuwakumbusha wataalamu wote juu ya namna mzuri ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa wakati ili kusaidia kupunguza athari
zinazoweza kujitokeza.
Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha pamoja na mgeni rasmi katika Kampasi ya Edward Moringe mkoani Morogoro |
0 Comments