Na:Tatyana Celestine
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wamekipongeza Chuo chao kwa kuona umuhimu wa kuwapatia Mafunzo kwa Vitendo kupitia maeneo yake ambayo yana Miundombinu rafiki ya kujifunzia kupelekea kupunguza gharama za usafiri, kuokoa muda, kujikimu pamoja na urahisi wa kujifunza kwakuwa karibu na walimu wao kwa kuwapa msaada papo kwa papo pindi wanapouhitaji.
Akizungumza na SUAMEDIA Bi.
Leila Kwigizile ambaye ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu Shahada ya Kilimo
cha Mboga na Matunda (Hortculture) amesema Mafunzo kwa Vitendo hasa
yanayohusiana na utafiti kufanywa karibu na walimu wao imewasaidia kuweza kujua mambo
mengi pia walimu wamekuwa wakiwafuatilia
kwa ukaribu kuona ni kwa namna gani utafiti wao umefanikiwa na kama kuna
changamoto imekuwa rahisi kwao kufanya marekebisho ili kufikia lengo.
Bi. Kwigizile ameendelea kusema faida wameiona kutokana na uamuzi huo
wanarithishwa utaalamu ipasavyo hata kama kuna jambo lilikuwa hawakulielewa darasani
basi kueleweshwa pale wanapokutana tena katika mafunzo kwa vitendo tofauti
na kutoka nje ya chuo au kukutana na Mwalimu wengine ambapo watashindwa kujua madhaifu
ya mwanafunzi kwa haraka na kumsaidia.
Aidha amaetoa rai kwa vijana ambao wanaona kilimo sio sehemu yao amesema vijana wanatakiwa wawe tayari na uthubutu kwani kilimo ni ajira ambayo
haina mipaka, zaidi wajiunge na SUA kupitia
huko kilimo ni tofauti kulinganisha na
wanavyoona huko mtaani watambue wanayo nafasi ya kueleweshawa kilimo kwa ukubwa
wake ikiwemo tafiti zinazosaidia kutatua changamoto mbalimbali pia ushauri wa
namna ya kupanda na kuchagua mbegu bora.
Naye Afisa Kilimo Muandamizi katika Idara ya Mimea Mipando na Bustani SUA Bw. Godwin Rwenzaula amesema utaratibu wa Mafunzo kwa Vitendo umeendelea kuboresha Mazingira ya Chuo na pia kuzalisha wataalamu wenye ujuzi thabiti kutokana na jitihada za walimu wao kusimamia kikamilifu na matokeo wanayaona pasi kuambiwa na watu.
0 Comments