Na, Tatyana
Celestine, Winifrida Nicholaus
Watu wenye
mahitaji maalumu wanatakiwa kujumuika katika jamii ili nao waweze kukabiliana
na hali zote kama serikali ilivyotaka shule zote zihusishe wanafunzi wa aina mbalimbali bila kujali hali zao kwa kuwataka kuendana na halisi pindi watakapomaliza masomo yao waweze kufanya kazi
na watu wa aina zote pasi ubaguzi.
Akizungumza na wanataaluma katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es - Salaam Dr. Lwimiko Sanga katika kuwajengea uwezo juu ya watu wenye mahitaji maalumu na kusema kuwa Shule zote na Vyuo vinatakiwa kuzingatia miundombinu stahiki kwa wote kwani wakati umefika Serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) imeamua wanafunzi wote waweze kupata elimu kwa usawa.
Dkt. huyo amebainsha kuwa mifumo ya Elimu aina mbili nchini imeleta changamoto kubwa kwa watu wenye mahitaji maalumu kushindwa kufanya vema katika masomo na pia kushindwa kuchanganyika katika jamii ambapo kupelekea utofauti katika kila hatua zao za kutafuta elimu kwani kuna watu wa aina tofauti kama vile wasiiona, watu wenye ulemavu wa macho, watu wenye ulemavu wa viungo na wengine ulemavu unawajia baadae katika miangaiko ya maisha.
Aidha ametaja
mifumo hiyo ya kielimu kama vile mfumo wa elimu maalum na mfumo rasmi ambapo hugawa wanafunzi kulingana na mifumo hiyo kitu ambacho kinapelea jamii kutengeneza namna isiyofaa ya kuwatambua kwa majina ikiwemo kilema, kiwete, kipofu, Zeruzeru na wasiosikia kwa ujumla majina hayo ni
kandamizi.
Amesema mafunzo
hayo yaliyotolewa kwa wanataaluma yawe chachu katika kuzingatia kuwatambua,
kuwasaidia kufikia malengo, kuwajali, pia kutafuta ufumbuzi wa changamoto
katika upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wao pamoja na kutengeneza usawa kwenye Vyuo, Jamii na Taifa kwa ujumla.
“Jamii
nyingine imekuwa ikiua Watoto walemavu kwa kuona ni laana ama mkosi….sisi wote
ni binadamu hatutakiwi kuonesha unyanyapaa kwani sote ni walemavu kwa namna
tofauti, kama tutapimwa kila mmoja atatambua lakini pia wengine ulemavu huja
kwa ajali, umri, kurithi na mengineyo” amesema Dr. Sanga.
0 Comments