Na: Tatyana Celestine, Winfrida Nicolaus
Wafanyakazi wametakiwa kuzingatia kupima Afya pamoja na ulaji unaofaa kwani ni jambo la muhimu kwakuwa mfanyakazi mwenye afya bora ni mtaji katika uzalishaji ambapo mwajili ananufaika kupitia yeye kwaweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu na ufanisi kufikia malengo ya Taasisi hata Taifa mahala pa kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Dkt. Erhard Kapilima kutoka Kurugenzi ya Huduma za Afya Hospitali ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) Tawi la SUA ambapo amesema elimu ya masomo yahusuyo Afya ni muhimu kwa wafanyakazi kwakuwa watatambua aina za magonjwa vilevile visababishi vya magonjwa hayo hasa yale magonjwa sugu yasiyoambukizwa ambayo mara nyingi yanatokana na mitindo ya maisha.
“La msingi magonjwa haya sugu yasiyoambukizwa yameongezeka kwa kiasi kikubwa na kusababisha nguvu kubwa ya utendaji kazi kupotea hivyo nitoe wito kuzingatia nidhamu ya ulaji kwa kuwa ndio tatizo kubwa vilevile utaratibu wa kufanya mazoezi na matumizi ya sigara pamoja na pombe kupita kiasi ni kati ya vitu vikubwa vinavyozorotesha afya na kuharibu kabisa utendaji kazi”, amesema Dkt. Kapilima
Dkt. Kapilima ameongeza kwa kusisitiza Chama cha Wafanyakazi THTU kimeatoa elimu ya afya kwa wanachama wake hivyo isiishie hapo yanapaswa kuwa endelevu kwakuwa ni chachu ya kufungua watu uelewa wao ili kuweza kuchukua hatua stahiki katika kuhakikisha afya zao zinakuwa imara katika kurahisisha utendaji kazi,
Amesema wafanykazi wanapotambua masuala hayo inawasaidia kuchukua hatua kujikinga na kuboresha afya zao zaidi kwenye mazingira ambayo wanafanyia kazi. na kwa yule ambaye anahisi anahitaji kujua zaidi Hospitali yao ya SUA inatoa huduma ya kuelimishs vilevile bado chuo kupitia hospitali inafadhiri vipindi vya redio kupitia SUA FM kuhusu masuala ya afya.
Kwa
upande wake Dkt. Prisila Mkenda Mhadhiri SUA kutoka Idara ya Sayansi ya Viumbe
Hai ambaye pia ni mwanachama wa THTU amesema wamekuwa na wakati mzuri kutokana
na mafunzo waliopatiwa yamekuwa ni ya msingi kwao hasa kwa upande
wa afya kuhusiana na namna gani wanaweza kujikinga na magonjwa sugu yasiyo ya kuambukizwa
ambayo yamekuwa ni tatizo sana kwenye jamii hivyo
kwa elimu hiyo itasaidia kubadili namna wanavyoishi.
“Tumekuwa
tukila vyakula ambavyo ni vya kisasa zaidi na kusahau vile vyakula vyetu vya
asili ambavyo pengine vina afya na manufaa mwilini kuliko hivi vya kisasa
vilevile tumekuwa ni watu ambao hatuna mazoezi Wala kutembea umbali wowote mara
nyingi tumekuwa tukitumia magari, kukaa ofisini, kula na kulala hivyo mafunzo
haya yametupa namna ya kutafakari na kubadili mienendo yetu ya maisha ili
kulinda afya zetu na kudanya kazi kwa uadilifu kwasababu afya zetu ni imara”,
amesema Dkt. Prisila Mkenda
0 Comments